WATU 7 WAUAWA KINYAMA KWA KUCHOMWA MOTO WAKITUHUMIWA KUWA NI WACHAWI

Watu saba wameuwawa vibaya kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kwa kuhusishwa na imani za kishirikina,huku nyumba ishirini zikichomwa moto katika kijiji cha Murufyiti,wiliaya ya Kasulu Mkoani Kigoma. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgYEMtOPqMRDUVWRLf8Xsdb6cDp0ryMaKV2roBAnEcd5aiYi0IzSRJ7VyI2bl6Ms5J96S-Mx5edoVuZ4fzL5vuvC6hiiuw_9ptxlZtHQYax6jF_7UG-BpEACJ0Ya2QqsYxCOW3g8JkKM8/s1600/6.jpg Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma,Japhari Muhamed amesema,tukio hilo lilifanyika juzi majira ya saa nne usiku baada ya M/kiti wa kijiji hicho aitwaye Evarist Ruhaya akishirikiana na mganga wa jadi,Faustino Ruchagula kupiga mbiu ya hatari ili kukusanya watu na kufanya unyama huo. .amesema watu waliouwawa ni ,John Muvuma (68),Elizabeth Kaje (55),Dyaba Kitwe (55),Vincent Ntiyaba (42),Helman Ntabiloye (78),Redamta Mdogo (60) na Ramadhani Kalaliza (70) wote wakiwa ni wakazi wa kjiji hicho cha Murufyiti,pia nyumba18 zilichomwa moto na zingine mbili kubomolewa na kutimiza idadi ya nyumba20. ....kamanda Mohamed amesema,tayari watu13 akiwemo mwenyekiti wa kijiji wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea kuhakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani. .....nae mtendaji wa kijiji hicho Ogeni Gaspa amesema kabla ya wauaji kuanza alipiga simu kwa OCD ili polisi waje kutuliza ghasia lakini gari hazikuwepo kituoni hivyo hali iliyopelekea Polisi kufika eneo la tukio kwa kuchelewa na kukuta mtu wa mwisho akiuwawa. ....kwa upande wa mtoto mmoja wa marehemu,aliejitambulisha kwa jina la Josiphat John amesema:-wakati tukio hilo linaendelea kwa wazazi wangu nilishindwa kutoka nyumbanikwangu kwa hofu ya kudhulika lakini ilipofika alfajiri nilikwenda kuangalia miili ya wazazi wangu ndipo nilipokuta imeteketezwa na moto... Mwisho wa Habari. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgqte6iBReyVwD55kz-qHhEfEIOaDpR4mCas0cTRXK6MaOH-jroZ18rvlw3AyNTIte2jVWQC65zGu4ePEQAkp1i4kqZd1P4RySmAzlg48wtVWhBoQlKBfOvR2BMKLx362ujaWfUX3UOY5E/s1600/8.jpg https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEic_BbmC3eG7PxURenmomy2BQa4mt5etO6v3eHxr_ZDNSzDO4k9WQlWPMdsAKl133hcU2Yhr8jHhSrZDvqVAaVn6OwShkR8ZUoYu-TiSE-XISMXNqUyW4FOd-2eqXIvPWORniy6rh4JV5U/s1600/9.jpg https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdcU6LLzyfc1xyHBJbxmi1TpZs4mkfSB6Wk-fltauI0C3MdF53Qiw75UiLBmRWT94uKzyercwOY8l5NszbbMWH9mbvbaZzNbd2EHVRFwKxNTgEOjc_PGAB0xgRmQRzKz9v0z7i1dI0Mok/s1600/11.jpg
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: