KITUO CHA POLISI LINDI CHANUSURIKA KULIPUKA WAKATI ASKARI WAKICHOMA MOTO TAKATAKA KITUONI HAPO

Kituo Kikuu cha Polisi cha Manispaa ya Lindi kimenusurika kuungua baada ya mlipuko kutokea wakati askari wakifanya usafi. Tukio hilo lilitokea jana saa 1:30 asubuhi. Imeelezwa kuwa askari hao walikuwa wakizichoma moto takataka ambazo zilikuwa na vitu vilivyolipuka. Mlipuko ulikuwa na kishindo kikubwa kiasi cha kusababisha taharuki kwa watu waliokuwapo kituoni hapo na maeneo ya jirani. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga alisema mlipuko huo ulisababishwa na chupa ambayo hata hivyo hakueleza ilikuwa na kitu gani kinacholipuka. “Kuna uharibifu umetokea. Vioo vya dirisha la ofisi ya mkuu wa kituo na chumba cha mashtaka vimevunjika kutokana na kishindo hicho,” alisema Kamanda Renata. Awali, kabla Kamanda huyo hajatoa ufafanuzi, taarifa zilizozagaa mitaa zilidai kuwa lilikuwa ni bomu linalotumiwa na wavuvi haramu wa samaki. Ilidaiwa kuwa lilikuwa limefichwa kwenye takataka zilizokusanywa nyuma ya kituo hicho. Baadhi ya watu pia walidai kuwa mabomu hayo ya kienyeji hutupwa hovyo mitaani hivi sasa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: