DIWANI ATUHUMIWA KUCHUKUA TOFALI ZA KUJENGEA MAABARA NA KWENDA KUJENGA NYUMBA YAKE BINAFSI
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata Chimala Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kimemtaka Diwani wa kata hiyo Hussen Vayahe (CCM) kuzirejesha tofali zaidi 2500 mali ya kata ambazo anadaiwa kuzichukua na kuamua kujengea nyumba yake binafsi pasipo kuwashirikisha wananchi.
Hayo yamebanishwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho kutoka Wilaya ya Mbarali Asajile Kajuni katika Mkutano wa hadhara wa kukijenga chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Isitu wilayani hapa ukiwa ni Mkutano wa saba katika Wilaya hiyo
Akiwahutubia mamia ya wananchi katika kijiji hicho Kajuni alimshutumu diwani huyo kutumia mali za wananchi kwa matumizi yake binafsi pasipo kuwashirikisha na kwamba kuna haja kwa diwani huyo chama cha mapinduzi kuchukuliwa za kisheria.
Kajuni alisema kuwa kwa zaidi ya mika miwili sasa diwani huyo alijichukulia uamuzi wa kutumia tofali hizo ambazo zilifyatulia kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Sekondari ya Mengele iliyopo katika kata hiyo ya Chimalana kwamba mpaka sasa ujenzi umesimama kwa sababu ya Diwani huyo.
‘Ndugu zangu lazima tuungane kuhakikisha huyu bwana anarejesha tofali zetu kwani haiwezekani nguvu za wananchi zikapotea bure,Diwani wetu amechukua tofali zetu amejengea nyumba kwa ajili ya mashine za kukoboa mpunga ili hali watoto wetu hawana maabara’alisema Kajuni
Alisema kuwa kitendo cha kuamua kuzitumia tofali hizo bila idhini ya wananchi ni dharau dhidi ya wananchi huku akidai kuwa alipewa ruhusa na kamati ya maendeleo ya kata, wakati hakuna kikao chochote kilicho keti wala muhutasari wowote unaonyesha kikaoo cha kuazima tofali hizo.
Katika Mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na viongozi wa chama hicho ngazi ya Mkoa Kajuni alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wafuasi wa chama cha Mpinduzi wakimtaka aachane na siasa kwa madai kuwa ameshakuwa na mafakio katika maisha lakini yeye amekuwa akigoma kwa madai kuwa hawezi kuacha siasa mpaka pale atakapo ona jamii ya wanachimala wawe na maisha mazuri.
‘Ndugu zangu kuna watu wananifauta eti niache siasa kwa kuwa nimesha kuwa na mafanikio, lakini kamwe sita acha siasa mpaka pale maisha ya wanachimala yatakapo kuwa safi’alisema Kajuni
Kwa upande wake mjumbe wa Kamati hamasa ya chama hicho Mkoa wa Mbeya Rose Mahemba aliwataka wanawake kutoka kata hiyo kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kaunzia nagazi ya Mitaa,Vitongji kata,pindi uchaguzi utakapo fanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha katika hatua nyingineMahemba alisema kila mwana jamii anapaswa kulivalia njuga suala la elimu kwa watoto kwa kike kwani hivi sasa mtaji wa chama cha mapinduzi ni wanawake na wengi wao hawana elimu ya kutosha na kwamba endapo wanawawake wakijitambua Tanzania itapiga hatua katika nyanja zote.
0 comments:
Post a Comment