ANGALIA PATASHIKA LA KUFA MTU BIBI AKIPAMBANA NA KIBAKA ALIYETAKA KUMUIBIA GARI LAKE
Deborah Smythe, 52, alisimamisha gari lake, akaacha mlango wazi huku bado linawaka, wakati akienda kufungua geti la kuingia kwenye kampuni yake.
Kibaka aliyekuwa karibu, akakimbilia na kuingia kwenye gari hilo na kujaribu kuliiba. Mama huyo alikimbia kurudi na kupambana na kibaka huyo.
Katika patashika hilo lililotokea jijini Manchester, UK, kuna wakati Beborah alianguka na nusura akanyagwe na gari hilo. Deborah alipata majeraha kama michubuko, lakini alifanikiwa kuokoa gari lake baada ya kibaka huyo kuona mhanga wake ni mbishi kuliko alivyotarajia, na kuamua kukimbia.
Mwanae Deborah, ambaye anajivunia ujasiri wa mama yake, amepost video hii Facebook na ujumbe ufuatao akiwasihi watu wasaidie kumtafuta kibaka huyo: “This scum bag tried robbing my mums car at 7:45am this morning outside her work!! (Ripponden road) She is pretty badly bruised but as you can see shes a lil warrior! Please please please if anyone recognises this man/his clothes or saw anything please we NEED to find this man !!!!!!”
0 comments:
Post a Comment