Mshindi wa mashindano ya Insha ya SADC afanyiwa hafra Makambako

Baada ya msichana Neema Mtwanga ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Naboti iliyopo mkoani Njombe kuibuka kinara wa mashindano ya Utunzi wa Insha katika nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) mwishoni mwa wiki iliyopita alifanyiwa hafra ya kumpongeza.
Hafra hiyo iliyojumuisha Wanafunzi wa shule hiyo, walimu, pamoja na shule za jirani wakiwemo viongozi wa dini kutoka mkoani Njombe, ilifanyika kwenye shule ya Naboti iliyopo Halmashauri ya Mji Makambako.
Akizungumza kwenye hafra hiyo, Mkurugenzi wa shule hiyo, Salon Mbilinyi aliahidi kumwendeleza kielimu msichana kwa kumsomesha kidato cha tano hadi cha sita mara atakapo hitimu kidato cha nne mwaka huu.
Pia aliahidi kutoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kugawana walimu wote wa shule hiyo.
Naye mgeni rasmi kwa niaba ya Afisa Elimu Halmashauri ya Mji wa Makambako, Aneth Mbajo alizitaka shule nyingine kuiga mfano mzuri wa shule ya Naboti yakufanikiwa kuibuka kinara kwenye shindano hilo.
Kwa upande wake, msichana Neema akizungumza kwenye hafra hiyo, aliwashukuru wanafunzi wenzake pamoja na walimu wake kwa ushirikiano mkubwa waliompa akiwa shuleni hapo.
Msichana Neema Steven Mtwanga, 16, aliibuka mshindi wa nafasi ya kwanza miongoni mwa washindani 39 waliowania Tuzo ya Utunzi wa Insha hiyo kwa Mwaka 2014.
Mtwanga ametunukiwa Tuzo ya ushindi huo katika Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC uliofanyika katika Hoteli ya Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe.
Nafasi ya pili imeshikwa na Kudzai Ncube kutoka Shule ya Sekondari ya Mazowe nchini Zimbabwe na nafasi ya tatu imeshikwa na Manxoba Msibi kutoka Shule ya Sekondari ya Etjendlovu katika Swaziland. Kwa ushindi huo, Neema Mtwanga ambaye yuko kidato cha nne, alizawadiwa hundi ya dola za Marekani 1500 ambayo ni sawa na shilingi milioni 2.3 na alilipiwa gharama zote za kumwezesha kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC ambapo alikabidhiwa zawadi hiyo.
Mbali na zawadi hiyo ya hundi, Neema alipewa zawadi ya ipad kwa ajili ya matumizi yake ya teknolojia ya mawasiliano na habari.
Mashindano hayo ya Insha ya Mwaka 2014 yalianzishwa rasmi Oktoba, 2013 ambako washindani walitakiwa kuandika Insha kuhusu mada: ?Climate Change is having adverse effect on the socio-economic development in the Region. What should the Education Sector do to mitigate the impact on the youth? ? Mabadiliko ya Tabia Nchi yanaathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Kanda ya SADC.
Nini Sekta ya Elimu ifanye kupunguza athari hizo kwa vijana? Insha 39 zilipokelewa kutoka nchi 13 kati ya nchi 15 wanachama wa SADC ikiwa ni Insha tatu kwa kila nchi.
Insha zilipokelewa kutoka Tanzania, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
Majaji wa kupitia na kuamua washindi wa Insha hizo walitoka Tanzania, Zambia na Zimbabwe na walikutana mjini Gaborone, Botswana, Julai, mwaka huu kupitia Insha zote na kutoa uamuzi wa nani washindi


Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment