Faida za bamia ni nyingi lakini tutakazozitaja hapa ni kuzuia kisukari, kusaidia katika ujauzito, kuondoa mada hatari mwilini zinazoweza kusababisha saratani na pia kuponya magonjwa kama asthma, kukohoa na matatizo ya kupumua Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambayo inafahamika na wengi katika jamii kutokana na ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo. Wapo wanaoitumia kama kiungo cha mboga na wengine huifanya mboga kamili. Bamia ina majina mengi, wengine huiita okra na kwa jina lisilo rasmi Kiingereza huitwa, 'lady finger' au gumbo. Bamia kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo maeneo makavu, na mboga hiyo imekuwa ikitumika kwa miaka mingi katika historia ya lishe na matibabu ya mwanadamu kutokana na faida zake nyingi kiafya. Bamia inajulikana kwa kuwa na kiasi kingi cha vitamin C, vitamin K na folic acid. Pia bamia ni maarufu kwa kuwa na ufumwele mwingi unaosaidia tumbo kusaga chakula vizuri na kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Si hayo tu bali bamia ina vitamini A nyingi ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu. Kwa kifupi, sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake. Vitamini A itokanayo na mboga hiyo husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi. Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara huimairisha mwanga katika macho yao. Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yanayotokana na virusi kama vile mafua. Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi. Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo. Kama tulivyosema vitamini K iliyopo kwenye mboga hiyo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu. Vitamini kadhaa zilizoko kwenye mboga ya bamia kwa ujumla tunaweza kusema inasaidia katika magonjwa mbalimbali. Uchunguzi umeonesha kuwa, kula bamia husaidia katika magonjwa ya figo. Katika uchunguzi huo imeonekana kuwa wale ambao wanapendelea kula bamia, mboga hiyo inaweza kuwakinga na ugonjwa wa figo. Kutokana na ufumwele mwingi iliyokuwa nao pia bamia huimarisha afya ya utumbo kwa kusaidia kusafisha mfumo wa kusaga chakula. Faida za bamia ni nyingi lakini tutakazozitaja hapa ni kuzuia kisukari, kusaidia katika ujauzito, kuondoa mada hatari mwilini zinazoweza kusababisha saratani na pia kuponya magonjwa kama asthma, kukohoa na matatizo ya kupumua

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: