PUMZIKA KWA AMANI MDOGO WETU IBRAHIM UBEPARI UMERUDI Si siasa jamani,ni kweli yametokea, Imeniuma jamani,jambo niloshuhudia, Kama mambo ya zamani,yale tuliyosikia, Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi. Mtu anafuga mbwa,si dhambi ninatambua, Anapendwa huyo mbwa,hata akija kuua, Kila siku anaomba,mbuzi wanateketea, Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi. Wengine kwenye mashamba,amani hawaioni, Mbuzi wetu kwenye nyumba,nje hakuna amani, Kweli mbwa kama simba,basi mweke mbugani, Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi. Juzi mwana ameua,kaua mwana mdogo, Eti watoa fidia ,waona ni jambo dogo, Ni mzaha waongea,kubwa walipa kisogo, Ubepari umerudi ,ubepari wa mweusi. Ashangaza huyu bwana,anavyofanya mzaha, Baba kamkosa mwana,ni kweli si mzaha, Polisi tumewaona,nanyi mwafanya mzaha, Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi. Vyovyote itavyosemwa,uzembe unachangia, Sio kamwa mwatukanwa,ukweli twawaambia, Leo mmevumiliwa,kesho msije kimbia, Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi. Pole kwenu wanafunzi,mlomzoea Ibu, Pia kwa wake wazazi,mungu atatoa jibu, Pia kwenu viongozi,mnaiona aibu, Uepari umerudi ubepari wa mweusi. PUMZIKA KWA AMANI MDOGO WETU IBRAHIM,,,,, source,,, kalam yangu

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: