URUGUAY imeanza vibaya Kombe la dunia baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Costa Rica usiku huu katika mchezo wa Kundi D Fortaleza, Brazil. Uruguay ilitangulia kupata bao la penalti la Edinson Cavani dakika ya 24 kabla ya kinda wa Arsenal, Joe Campbell kuisawazishia Costa Rica dakika ya 54. Huku mshambuliaji nyota wa Uruguay, Luis Suarez ambaye ni majeruhi akiwa benchi, alishuhudia jahazi la timu yake likizama kwa mabao mawili zadi kipindi cha pili. Oscar Esau Duarte aliifungia Costa Rica bao dakika ya 57 kabla ya Marcos Urena kufunga la tatu dakika ya 84. Maxi Parera alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei kwa kumchezea rafu Campbell.

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: