Kocha mtarajiwa wa Yanga, Marcio Maximo ndiye atakuwa anapendekeza wachezaji anawaowataka kwa ajili ya kuboresha kikosi chake. Taarifa zinaeleza, baada ya Maximo kuomba apewe nguvu ya mwisho kwenye usajili, Yanga imekubali kumkabidhi. Habari za uhakika kutoka kwa upande wa wakala anayeshughulikia ujio wa Maximo zinaeleza sasa atakuwa akipendekeza na kusajili wachezaji anaoamini watakisaidia kikosi chake. “Sasa makubaliano ni asilimia zaidi ya 95, wakati wowote anakuja na tayari kocha ameomba kupewa rungu la usajili na imekubalika,” alisema. Maximo ndiye kocha mtarajiwa kuziba pengo la Hans van der Pluijm, raia wa Uholanzi ambaye ameondika baada ya kupata dau la juu. Lakini imekuwa ikielezwa wachezaji wa Yanga wamekuwa na hofu kuhusiana na ujio wake na hasa Juma Kaseja na Athumani Iddi Chuji ambao wamekuwa hawaelewani. Lakini uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa bado uko kwenye mazungumzo na kocha huyo na masuala mengine yote yanawezekana

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: