HATARI KWA FAMILIA ZINAZOTUMIA MAZIWA HAYA KWA AJILI YA WATOTO

i wish you happy chrismass and happy new year

Familia zinazotumia maziwa ya kopo aina ya Lactogen,ambayo yamesajili hapa nchini kwa ajili ya kutumiwa na watoto wachanga,zina hali ngumu baada ya kuadimika,huku ikielezwa kuwa yatazidi kuadimika kwa zaidi ya miezi miwili ijayo.

Uchunguzi umebaini kuadimika kwa maziwa hayo yanayotengenezwa nchini Ufaransa kunafanya baadhi ya familia kununua kwa bei kubwa na wengine kulazimika kubadili aina ya maziwa kwa watoto wao.

Mmoja wa wauzaji wa maziwa hayo kwa rejareja alisema tatizo hilo lilianza kujitokeza mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana na kufanya bei yake kupanda kutoka 15,000 kwa kopo hadi 20,000.

Kwa upande wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kupitia Ofisa habari wake Gaudensia Simwanza mamlaka yake inasimamia ubora wa bidhaa za maziwa ya watoto na wamekua wakiendesha operesheni ya kuondoa bidhaa hizo feki.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: