WALIMU TUNDURU WATISHIWA BAADA YA KUSHIRIKI KATIKA MGOMO

Na Mwandishi wetu, Tunduru. WALIMU wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, ambao walishiriki kwenye mgomo uliolitikisa taifa, wametishiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na hata kuwajibishwa endapo itabainika walifanya hivyo. Ofisa Elimu wa wilaya hiyo Rashid Mandoa, alisema kuwa walimu hao watachukuliwa hatua za kuwajibishwa, kutokana na kukiuka taratibu za kufanya mgomo na watahesabiwa kama watoro katika siku walizoshiriki mgomo huo. Akifafanua tukio hilo, alisema walimu hao watatakiwa kujutia kitendo hicho kutokana na kupotoshwa na uongozi wa Chama cha Walimu (CWT). Mandoa alisema tayari wamekwishatuma timu ya waratibu elimu kata na makatibu kata kutembelea shule zote wilayani humo, ili kubaini walimu walioshiriki mgomo huo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: