TANZANIA, UGANDA WAKIMBIZA KRIKETI GYMKHANA
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo Kriketi chini ya Umri wa miaka 19 ilishiriki mashindano ya dunia ya ICC nchini Zambia kuanzia tarehe 8 -18 Agosti 2014.
Michuano ya kimataifa ya mchezo wa kriketi kwa wanawake chini ya miaka 19, imeanza kutimua vumbi kwenye viwanja vya Gymkhana pamoja na Annadil jijini Dar es salaam Tanzania.
Mashindano hayo yanashirikisha nchi sita ambazo ni wenyeji Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Botswana, pamoja na msumbiji.
Mchuano hii inafanyika kwa mara ya pili jijini Dar es saalam kwa Tanzania kuwa wenyeji, ambapo itachukua muda wa siku tatu kuanzia 7/12/2014 mpaka tarehe 9/12/2014.
Uganda ndio wanalishikilia kombe hilo Kwa kuwa mabigwa watetezi baada ya mwaka jana kufanikiwa kuibuka mabingwa na kukabidhiwa kikombe hicho.
Michezo iliyochezwa mapema jana kwenye uwanja wa Annadil Kenya waliwafunga Botswana kwa mikimbio 109 dhidi 97.
katika mchezo wa pili Kenya wakawabugiza Rwanda kwa mikimbio 94 kwa 31 na mchezo wa mwisho Rwanda wamewabanjua Botswana kwa mikimbio 68 dhidi ya 67.
Kwenye uwanja wa Gymkhana mchezo wa kwanza msumbiji aliadhibiwa na Uganda kwa mikimbio 103 dhidi ya 29, Huku wenyeji Tanzania wakiwachapa msumbiji kwa mikimbio 100 kwa 34 na mchezo wa mwisho Tanzania wameambulia patupu kwa kufugwa kwa mikimbio 65 kwa 63 dhidi ya Uganda.
Michezo hiyo itaendelea tena leo mchezo wa mapema asubuhi kwenye uwanja wa Gymkhana utawakutanishana Kenya na Msumbiji, mchezo wa pili utakua kati ya Tanzania na Kenya, mchezo wa mwisho wenyeji Tanzania watachuana na Rwanda.
Wakati kwenye uwanja wa Annadil mchezo wa kwanza Uganda watachuana na Rwanda, mchezo wa pili Botswana watapepetana na Uganda, na mchezo wa mwisho utawakutanisha Botswana dhidi ya Msumbiji
0 comments:
Post a Comment