BALOTELLI AKUTWA NA HATIA, APEWA HADI DESEMBA 15 KUJIBU MASHITAKA
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekuwa na hatia na Chama cha Soka England baada ya kuposti picha inayodaiwa ya udhalilishaji kwenye mtandao wa kijamii.
FA imesema Balotelii amekutwa na hatia kwa kuvunja sheria E3 (1) na Mtaliano amepewa hadi Saa 12:00 jioni ya Desemba 15 kusema namna gani atajibu kesi yake.
Balotelli anakabiliwa na adhabu kama ya beki wa QPR, Rio Ferdinand ambaye kwa kuvunja sheria E3 Oktoba mwaka huu, Nahodha huyo wa zamani waManchester United alifungiwa mechi tatu na kupigwa faibi ya Pauni 25,000 kwa kuweka picha ya udhalilishaji kwenye akaunti yake ya Tweeter. Ferdinand pia aliwahi kutozwa faini ya Pauni 45,000 mwaka 2012 kwa kumdhalilisha beki wa wakati huo wa Chelsea, Ashley Cole akimuita 'choc ice' kwenye Twitter.
Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli amekutwa na hatia na FA kwa picha ya utata aliyoposti kwenye akaunti yake ya Instagram
0 comments:
Post a Comment