TFF YATIA BARAKA KIEMBA KUIFUNGA SIMBA

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba ambaye ameenda Azam FC kwa mkopo Amri Kiemba anaruhusiwa kucheza mechi yoyote ya ligi kuu itakapoanza Desemba 26. Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa mashindano ya TFF Boniface Wambura kufatia maswali mengi ya wadau kuwa itakuwaje Azam na Simba zitakapokutana au timu ambazo kiemba alikutananazo akichezea Simba na huku akikutananazo akiwa Azam?. Majibu ya Wambura yalimpatia baraka Kiemba kucheza atakavyo kutokana na sheria za uhamisho zinafahamika maana tayari atakuwa ni mchezaji wa Azam lakini kwa mkopo akiwa ni mali ya Simba. Mfano, Kiemba alicheza katika mechi ya Simba na Coastal Union hivyo siku Azam itakapokutana na Coastal au Simba mchezaji huyo atakuwa na ruhusa ya kucheza mchezo wowote.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: