LUDEWA NA CHANGAMOTO YA MAENDELEO
LUDEWA NA VIKWAZO VYA MAENDELEO.
Na.barnabas njenjema
LUDEWA,
Historia inaonesha tatizo kubwa la wananchi wa Ludewa ni
miundombinu, mawasiliano na nishati.
Lakini Ludewa tunakasumba ya utengano tuwapo katika sekta fulani licha ya kuwa tunapiga stor pamoja.
Mfano.
Hospitali yetu ya wilaya ya Ludewa pamoja na shule yetu ya Chief kidulile ina upungufu mkubwa wa wafanya kazi ila cha ajabu vijana wapo mtaani na wanataaluma hizo ila wanakosa nafasi za kufanya kazi katika idara izo.
Sekta binafsi pia matatizo kama hayo yapo kisa tu wewe mzaliwa wa hapa tuache roho mbaya wapendwa..
Licha ya uwepo wa fulsa mbalimbali za kiuchumi haya yamekuwa matatizo sugu katika wilaya ya Ludewakitu kilichopelekea fulsa hizo kutofanyiwa kazi mfano wa fulsa hizo ni kilimo, ufugaji, uvuvi, vivutio vya utalii vya milima ya livingstone na misitu ya asili ya Milo,Madini maeneo ya amani, Mgodi wa chuma cha Liganga na makaa ya mawe ya mchuchuma maporomoko ya mito mfano mnyereri.Mabaki ya vitu vya kale kwakibaba [utilili] na tamaduni za watu wa Ludewa ngoma ya mganda.Tangu kuwepo kwa mbunge Deogratias Filikunjombe baada ya wananchi wa Ludewa mkoa mpya wa Njombe wana matarajio makubwa sana ambayo yametokana na mbunge kutimiza ahadi mbalimbali wilayani Ludewa.kubwa kutia saini mkataba wa ufuaji wa chuma cha liganga na makaa ya mawe ya mchuchuma.ni jambo nzur ila tujiulize je kutaweza leta mabadiliko ikiwa vijana na wananchi wa Ludewa hawana elimu juu ya migodi hiyo?.
Ni vyema sasa wahusika wahakikishe vijana wao wanapata elimu mapema kama ufundi wa aina mbalimbali kwani migod hiyo lazima itaanza na ujenzi wa nyumba lakin cha ajabu utaona hata mafundi kujenga watatoka nje ya Ludewa.
Tatizo la barabara limekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa miaka mingi kwa mwaka huu hatua ya kupanua barabara na kukarabati kwa kiwango cha changarawe na baadae kuweka rami toka Njombe hadi Manda.pamoja na barabara za mitaa hapa Ludewa mjini kujengwa kwa kiwango cha rami kunaleta matumain kwa wanachi.
Kukamilika kwa bara bara hizo pia kutapelekea fulsa mbalimbali kama utalii kutofanyiwa kazi hivyo kuboresha serikali mapato. Tatizo la mawasiliano lipo ila ni kiwango kidogo kwani sehemu mbambali makampuni ya simu yameweza kufikisha mawasiliano
Nishati ya umeme pia ni tatizo kwani hadi mwaka 2014 unakamili kuna vijiji vingi bado havina nishati ya umeme licha ya juhidi za mh.mbunge kufikisha umeme kila mahari ikiwa pamoja na Luana na Lupingu,na vijiji vya miliman ila ndugu zangu wa manda tumesahaulika.
Tatizo lipo katika kata za Mlangali Lupanga,Masasi na mwambao mwa ziwa nyasa hasa kata ya manda ambapo hakuna umeme hivyo uvuvi umekuwa hauna tija kwa taifa ambapo wavuvi wamekuwa wakifanya uvuvi kwa ajili ya kitoweo na kujikimu. Pia tatizo hili limepelekea watu washindwe kufungua viwanda vya kusindika matunda kwa sehemu ambazo matunda yanastawi matokeo yake matunda yanaagizwa kutoka Afrika Kusini.
Uwepo wa hospitali za madhehebu mbalimbali ya dinikama hospitali ya Lugalawa na hospitali ya milo pia Hospitali ya wilaya ya Ludewa na baadhi ya vituo vya afya kama mlangali na zahanati mbalimbali katika vijiji mbalimbali kwa kiwango Fulani kumewezesha watu wa Ludewa kupata huduma za afya lakini changamoto ni miundo mbinu mfano Kutoka Utilili mpaka hospitali ya Lugarawa zaidi ya 36km ni mbali sana pia barabara ni mbovu sana.
Licha ya wilaya ya Ludewa kutoa watu waliotikisa nchikatika Nyanja za siasa na taaluma kamaHayati Horace Kolimba, Mchungaji Christopher Mtikila, hayati Dr. Crispin Mponda na Prof Raphael Mwalyosiwilaya ya ludewa haina muamko wa kisiasa pia haina muamko katika suala la elimu hinatokana na kukosa expose na walioendelea kutorudi kwao kutoa msukumo wa mambo hayo. Jimbo la uchaguzi na wilaya la Ludewa ina mbunge wa CCM aliyepita bila kupingwa pia madiwani wawili wa upinzani [TLP] kwa lupingu na CHADEMA kwa mlangali hivyo hakuna changamoto za kutosha katika kuendesha halmashauri hiyo .
Hadi sasa wilaya ya Ludewa Na mpaka sasa wilaya hii haina chuo chochote cha taifa licha ya serikali kuahidi ujenzi wa chuo cha veta maeneo ya liganga ambapo mpaka sasa imekuwa ni ahadi na wanachi wanahoji na kuuliza ni lini ujenzi huo utaanza.
Changamoto hizi zimepelekea vijana wengi kukimbilia mjini kutafuta kile wengi wanachokiita kutafuta maisha lakini kwa miundombinu duni hata wananchi wa Ludewa wanaofanya kazi nje ya Ludewa wamekuwa wakikukataA kwamba sio kwao na wengine wamekuwa wakiishi mijini kwa miaka nenda rudi bila kurudi kwao.wafanyakazi ambao wamekuwa wakipangiwa kwenda Ludewa ama walimu ama madaktari na wengineo wamekuwa hawataki kwenda au wamekuwa wakiripoti na kurudi kwao.Pia imani za kishirikina ambazo huendekezwa baadhi ya maeneo zimepelekea wataalamu hao kutopenda kwenda Ludewa.
Sababu nyingi ila mojawapo ya sababu hizo ni pamoja na kutothaminiwa kwa mfanyakaz na kufanya kaz hapa sio sir wana ludewa tunakasumba na wivu ambao hadi leo ndio unatufanya tushindwe kusonga mbele kwa maendeleo.
Tuache wivu tujenge umoja tuibadili ludewa yetu.
0 comments:
Post a Comment