DEREVA TOYO sehemu ya 7 b
Inaendelea
Nilifika kisha nikabisha hodi na kumkuta mzee anaikagua hio pikipiki
"shkamoi mzee?"
"marahaba Aaahhh kijana karibu bwana"
"asante mzee"
"naona ndio umekuja sasa kijana?"
"ndio mzee...maana si unajua haya maisha?"
"Sasa kijana? mimi nitakupa hii pikipiki ila nahitaji hesabu ( malipo ) yangu isilale"
"aaahh sawa nitajitahidi ila nadhani hata wewe mzee unajua kua kuna siku mambo hayawi mazuri kikazi"
"najua hilo ila isiwe ikawa ndio wimbo....maana nimenunua ili inilipe na mimi"
"ondoa shaka mzee"
"sasa pikipiki utairudisha saa 3 kamili usiku na utaichukua saa 12 asubuhi sawa kijana?"
"sawa mzee.....kwahio kesho nije kuichukua eeh?"
"ndio maana yake..... ila zingatia hesabu yangu kijana"
"na si unajua ni pesa ngapi?"
"ndio mzee si Elfu saba mzee?"
"ndio hio ila biashara ikiwa nzuri tutaongea zaidi"
"sawa mzee wangu.....haya mi ngoja nitoke"
"haya kijana"
Sasa nilipotoka kwa mzee na sasa nipo njiani.... mara simu yangu ilipigwa...kucheki namba naona ni namba mpya kabisaa
Niliona bora nipokee maana huenda ikawa ni simu ya kazi
"hallo?"
"eee mambo?"
Ilikua ni sauti ya kike ila sikuwahi kuisikia
"poa tu nani mwenzangu?"
Nilimuuliza hivyo huku nikiisikilizia hio sauti kama naijua
"jamani umenisahau?"
"Tafadhali naomba useme shida yako maana tupo kikazi zaidi"
"ok mi nataka unipige picha?"
"upo maeneo gani wewe?"
"nipo sakina kibanda maziwa"
"ok tukutane wapi?"
"njoo hadi pale sakina baa utanikuta"
"poa nakuja sasa hivi"
Kama kawa nilikua na kamera yangu kwa ajili ya kupiga picha... nilikodi toyo mara moja na kupelekwa maeneo hayo....... kwakua tulitumia toyp hivyo haikua safari ndefu sana..... tulifika kisha nikaanza kuangaza macho huku na kule ili nimuone huyo alioniita...... Sasa kutupa macho vizuri Daahh sikuamini macho yangu kama ni yeye kweli.... nilimsogelea karibu na kumsalimia
"mambo?"
"poa nambie?"
"safi tu...vp wewe ndio ulioniita hapa?"
"ndio kwani vp?"
"aahh hakuna tabu.. na tupige hizo picha basi fasta"
"wala tu staki picha"
"kwanini sasa?"
"unajua nimekuitia nini?"
"sijui"
"basi tupande gari twende"
Kwakua mtoto wa kike alikua ni mzuri tena wakujiheshimu.... nilimkubalia maana hata mimi kamoyo kameshagonga kwake.. Sasa tulipoingia kwenye gari mtoto alikua anafunga mlango wa gari huku katisheti chake kakainuka kidogo nikaona kiuno kilaiiiiiiniiiiiiiiii Daahhh nilishawishika kukigusa.. maana sijawahi kuona kiuno kama hiki
"bwana wewe jemsi mbona hutulii?"
Heee nilijua nitafokewa kwa kumshika kiuno bila ridhaa yake... kumbe ndio nazidi kulembesha mzigo...Afu mtoto alivaa suruali nyepesiiiiiiii mpaka raha yani....
Sasa mtoto wa kiume si nikanogewa kushika kiuno..... kumbe alikua analoku milango ya gari kisha akanigeukia na kusema
"nilikua nakutega tu uingie kwenye himaya yetu.... sasa hapa hutoki na utulie hivyo hivyo nipige simu kwa mkuuu"
"haaaa kwani nimefanyaje jamani?"
"utajulia mbele ya safari"
Aliwasha gari na kulitoa mbiooooo
0 comments:
Post a Comment