LUDEWA CEMENT YATARAJIWA KUANZISHWA LUDEWA WAWEKEZAJI WA KAMPUNI YA KICHINA HWTZ KWA WANANCHI WA LUPANGA NA MASIMBWE


Katika juhudi za kukuza uchumi wa Wilaya ya Ludewa kupitia rasilimali zake kama chuma na makaa ya mawe, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas, amefanya mikutano ya hadhara katika vijiji vya Lupanga na Masimbwe kwa lengo la kuwatambulisha wawekezaji kutoka kampuni ya HWHG ya China. Kampuni hiyo imeanzisha kampuni tanzu nchini Tanzania kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) inayoitwa HWTZ, ambayo inapanga kuwekeza katika ujenzi wa viwanda mbalimbali wilayani humo.

Miongoni mwa viwanda vinavyotarajiwa kujengwa ni kiwanda cha saruji, ambacho kitazalisha bidhaa itakayojulikana kama "Ludewa Cement." Mhe. Thomas aliwahakikishia wananchi kuwa maeneo yao yatakayotumika kwa uwekezaji huo yatazingatia haki na fidia stahiki, na kwamba serikali itasimamia mchakato huo kwa uwazi na ushirikishwaji wa jamii.

Uwekezaji huu wa viwanda utahusisha baadhi ya vijiji katika wilaya hiyo, ambapo Mhe. Thomas alieleza kuwa mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na ajira, maendeleo ya miundombinu, na fursa za biashara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Ndg. Sunday Deogratius, aliwataka wananchi kutumia fursa za kibiashara zitakazojitokeza kutokana na uwekezaji huo, kama vile usambazaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa viwanda hivyo.

Wananchi waliohudhuria mikutano hiyo walieleza furaha yao kwa kuwapokea wawekezaji hao, wakielezea matumaini yao kuwa uwekezaji huo utaleta maendeleo na kuboresha maisha yao kwa ujumla.

Uwekezaji huu unatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi katika Wilaya ya Ludewa, na kuchangia katika juhudi za serikali za kukuza sekta ya viwanda nchini.










Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: