Ludewa, Njombe - Tarehe 1Mei 2025
Katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Mkoa wa Njombe umefanya sherehe hizo katika Wilaya ya Ludewa, ambapo tukio hilo limehudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi dkt. Pindi Chana, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, viongozi vya chama cha mapinduzi wilaya na mkoa,viongozi mbalimbali wa serikali, sekta binafsi, wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Njombe mkurugenzi na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya ludewa. Tukio hilo limepokelewa kwa shangwe na furaha kubwa kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, alieleza kuwa Rais Samia ameongeza kiwango cha mshahara ambapo kima cha chini cha mshahara kitakuwa ni Tsh 500,000 kutoka Sh. 370,000 iliyokuwa awali.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, aliwataka waajiri kuwapa wafanyakazi wao stahiki zao kwa wakati ili kuepusha migogoro isiy
o na tija. Pia alihimiza wananchi kuwekeza katika kilimo na biashara, akisisitiza kuwa vijana wanapaswa kuelekezwa katika maeneo haya kwa maendeleo ya taifa.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas, aliwashukuru wote waliohudhuria maadhimisho hayo na kuomba kwamba upendo uliooneshwa Ludewa siku ya Mei Mosi uendelee kuonekana katika wilaya zote za mkoa wa Njombe katika maadhimisho yajayo.
Maadhimisho hayo pia yalienda sambamba na utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora, ambapo mmoja wa waliopokea zawadi hizo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Mhe. Sunday Deogratias.
0 comments:
Post a Comment