Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk.Charles Msonde ametoa ripoti kamili ya ufaulu wa wananfunzi wa kidato cha pili, ambapo ameeleza kuwa wasichana wote wameingia kumi bora ya wanafunzi waliofaulu vizuri.
Aidha amezitaja shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo na kuipongeza shule ya sekondari Canossa kwa kufanya vizuri ambapo kuanzia nafasi ya tatu hadi nafasi ya nane imeshikwa na wanafunzi kutoka shule hiyo.
Shule zilizofanya vizuri, zilizoingia kumi bora ni
- Feza Girls na Shamimu Abdallah Mohamed
- Feza Girls na Rukia Hamisi Abdallah
- Canossa na Jacqueline Mbarwa Kivuyo
- Canossa na Marina Emmanuel Kashumba
- Canossa na Cate Penia Mgambo
- Canossa na Sylivia Titus Tibenda
- Canossa na Zuhura Hassan Sapi
- Canossa na Gladys Mokili Maluli
- Elizabeth na Emmanuel Kimaro
- Magdalena Weraufoo Munisi
Kufuatia matokeo hayo shule binafsi zimeibuka kidedea huku Tanga, Mtwara, Lindi na Ruvuma zimetoa matokeo mabaya na kupelekea kushika mkia ambapo Tanga imetoa shule 6 zilizioingia kumi bora kushika mkia.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment