ATLETICO KUFUZU UEFA UKO HAPA


Kikosi cha Liv­erpool
BARCELONA, Bayern, Chelsea, Beşiktaş, Man­chester City, PSG, Real Madrid na Tottenham tayari zilishafuzu hatua ya 16 bora lakini kuna timu nyingine 14 zinazowania nafasi nane zilizobaki katika michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mab­ingwa Ulaya itakayochezwa kesho na keshokutwa Jumatano.

Mambo ni magumu sana kwa baadhi ya vigogo, tazama jinsi hali ilivyo:
Zinazoweza kufuzu: Atlético Madrid, Basel, CSKA Moskva, Juventus, Leipzig, Liv­erpool, Manchester United, Napoli, Porto, Roma, Sevilla, Shakhtar Donetsk, Spartak Moskva, Sporting CP.
Ambazo haziwezi kufuzu: Anderlecht, APOEL, Borussia Dortmund, Celtic. Zitakazomaliza mkiani: Benfica, Feyenoord, Maribor, Monaco, Olym­piacos, Qarabağ.
MECHI ZA KESHO JU­MANNE
Kundi A: Manchester United (pointi 12) v CSKA Moskva (9), Benfica (0) v Basel (9)

Manchester United itafuzu ikiwa kileleni kama itapata poin­ti (na inaweza kufungwa 6-0 na bado ikafuzu). Kama Manches­ter itapoteza dhidi ya CSKA, na Basel ikashindwa kushinda dhidi ya Benfica, basi United na CSKA zitafuzu huku nafasi ya kwanza ikitege­mea nani alivuna pointi nyingi zaidi wal­ipokutana ‘head to head’ (United ilishinda 4-1 Urusi na itakuwa na uwiano mzuri zaidi wa mabao hata ikifungwa 4-1 kesho).

Kama CSKA na Basel zitashinda, basi nafasi mbili za juu itategemea ulinganifu wa nani alivuna pointi nyingi zaidi timu hizo tatu zilipokutana, ‘head to head’. Ikitokea hali hii, United watafuzu labda wafungwe 7-0, na watakuwa vinara labda wafungwe 5-0.

Basel watafuzu kama wak­iwa na matokeo mazuri zaidi ya CSKA au kama timu zote zikifungwa ama kutoka sare, kwa sababu Basel wana pointi nyingi zaidi timu hizo zilipokutana ‘head to head’.

Kundi B: Bayern (12) v PSG (15), Celt­i c (3) v Anderlecht (0)

Paris na Bayern zote zilishafuzu, huku nafasi ya kwanza ikitege­mea mchezo baina ya timu hizo. Paris ilishinda mchezo wa kwanza 3-0 na pia inaongoza kwa uwiano mzuri wa mabao, hivyo Bayern inatakiwa ishinde kwa tofauti y a m a b a o m a n n e ili imalize kinara.

Celtic na Anderlecht, m m o j a w ap o anaweza ku­maliza katika nafa­si ya tatu. Anderlecht walifungwa na Celtic 3-0 nyumbani, kwa hiyo Wabelgiji hao watalazimika kushin­da kwa tofauti ya ma­bao matatu jijini Glas­gow ili kufuzu Europa (kama wakishinda 3-0, Anderlecht watamaliza nafasi ya tatu kutokana na uwiano mzuri wa mabao walionao).

Kundi C: Roma (8) v Qarabağ (2), Chelsea (10) v Atlético (6)
Chelsea walishafuzu. Watathibitisha nafasi ya kwanza kwa ushindi au kwa matokeo yoyote yale kama Roma ikishindwa kushinda.
Roma itafuzu kwa ush­indi, au kwa matokeo yoy­ote kama Atletico Madrid itashindwa kushinda. Kama Roma ikishinda, na Chelsea ikashindwa kushinda, basi Roma watakuwa vinara.
Atlético wenyewe, ili wamal­ize katika nafasi ya pili, wanataki­wa kushinda na kutegemea Roma haishindi (kama Atletico na Roma wakimal­i z a na pointi tisa, Atletico itafuzu kutokana na kuwa na pointi nyingi timu hizo zilipokutana ‘head to head’). Qarabağ haina mjadala, ita­maliza ya mwisho.


Kundi D: Olympiacos (1) v Juventus (8), Barcelona (11) v Sporting (7)
Barcelona walishafuzu kama vi­nara. Juventus watafuzu kwa ushindi au kwa matokeo yoyote kama Sporting watashindwa kushinda (kama wakimal­iza pointi sawa, Juve itafuzu kwa uwiano mzuri wa head-to-head).
Sporting lazima ishinde, na itatinga 16 bora kama ikishinda halafu Juven­tus ikashindwa kushinda. Olympiacos watamaliza mkiani.

MECHI ZA JUMATANO
Kundi E: Maribor (2) v Sevilla (8), Liverpool (9) v Spartak Moskva (6)
Liverpool inahitaji sare tu ili ifuzu, na itajithibitishia nafasi ya kwanza kwa ushindi, au kwa sare kama Sevilla isi­poshinda. Kama Liverpool ikifungwa, itatupwa nje labda Sevilla nayo ifungwe (maana Liverpool itakuwa ya tatu kama timu zote zikilingana pointi, kutokana na uwiano wa mabao ya head to head).
Sevilla itafuzu kwa sare, au kwa ma­tokeo yoyote kama Spartak isiposhinda. Sevilla itashika nafasi ya kwanza kama ikishinda halafu Liverpool isiposhinda.
Spartak itafuzu kwa ushindi lakini itashika nafasi ya tatu kwa matokeo yoyote. Kama Spartak ikishinda itama­liza kileleni labda Sevilla nayo ishinde. Maribor haiwezi kujikwamua mkiani.

Kundi F: Feyenoord (0) v Napoli (6), Shakhtar Donetsk (9) v Manchester City (15)
Man City walishafuzu kama vinara. Shakhtar watafuzu kama wataepuka kipigo au kama Napoli isiposhinda.
Napoli yenyewe lazima ishinde halafu itegemee Shakhtar ipoteze; katika mazingira hayo, Napoli ita­maliza ya pili kwa faida ya head to head. Feyenoord haitaweza kutoka mkiani.

Kundi G: Porto (7) v Mo­naco (2), RB Leipzig (7) v Beşiktaş (11)
Beşiktaş wame­shafuzu kama vi­n a r a . P o r ­t o watafuzu k a m a wak­ishinda
au ikiwa tu wa­talingana pointi na Leipzig kutokana na faida yao ya head to head.
Leipzig lazima ipate pointi nyingi za­idi ya Porto ili kumaliza ya pili. Monaco iliyofika nusu fainali msimu uliopita, haitatoka mkiani.

Kundi H: Real Madrid (10) v Dort­mund (2), Tottenham (13) v APOEL (2)
Tottenham walishafuzu kama vinara kwa faida ya head to head dhidi ya Ma­drid. Madrid ilishafuzu kama mshindi wa pili. Dortmund na APOEL zitawania nafasi ya tatu. Ikiwa mwisho wa siku timu hizo zitalingana pointi, Dortmund itafuzu kutokana na uwiano mzuri wa mabao katika mechi zote.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: