Tottenham na R Madrid zawika, Livepool yazuiwa


Mshambuliaji Harry kane alifunga mabao mawili huku Tottenham ikiishinda Borussia Dortmund na hivyobasi kupiga jeki matumaini yao ya kombe la vilabu bingwa Ulaya katika uwanja wa Wembley.Umahiri wa kane mbele ya goli ndio tofauti kubwa waliokuwa nayo Suprs ambao kwa kipindi kirefu cha mchezo huo walilazimika kulinda lango la kutokana na mchezo mzuri ulioonyeshwa na vijana wa Dortmund.Bao lake la kwanza liliwawacha Dortmund bila jibu baada ya kutamba nampira kutoka upande wa kushoto wa uwanja kabla ya kucheka na wavu dakika 15 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la dakika ya 11 la Son Hueng-min kusawazishwa na mshambuliaji wa Dortmund Andriy Yarmolenko.Bao la pili la Kane ulikuwa mkwaju wa kimo cha nyoka katika dakika ya sitini na hivyobasi kuipatia timu yake motishaya kukabiliana na tishio la wapinzani wao waliotawala mechi hiyo.Hatahivyo Tottenham walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji 10 baada ya bekiJan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshika mchezaji wa ziada wa Dortmund Mario Gotze.

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: