Godbless Lema: Tundu Lissu bado Yupo ICU

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye sasa yupo Kenya amefunguka na kueleza kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu sasa ina afadhali ukilinganisha na hali aliyokuwa nayo siku mbili zilizopita ila amedaimpaka sasa bado yupo ICU.Lema amesema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na BBC Swahili  na kudai kuwa hali ya kiongozi huyo inazidi kuimarika ukilinganisha na siku za awali ambazo alikuwa amefanyiwa shambulio hilo."Mgonjwa anapokuwa yupo hospitali tena kwenye chumba cha wagonjwa mahututi huwezi kusemahali ya mgonjwa ni nzuri lakini kwa kadri ambavyo tumekuwa hapa Nairobi kwa siku zote mimi na wenzangu akiwepo Mchungaji Msigwa, mke wa Lissu na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe tunaweza kusema kuna mabadiliko lakini bado Tundu Lissu yupo ICU na ni wito wetu kwamba Watanzania wote wenye mapenzi mema waendelee kumuombea Tundu Lissu " alisema Godbless LemaAidha Lema anasema kuwa jaribio la kutaka kumuuwa Lissu ni mpango na watu waliofanya hivyo siyo majambazi bali walifanya hivyo kwa lengo la kutaka kutuma ujumbe kuwa wanaweza kufanya lolote na wasifanywe jambo lolote.Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya kupatiwa matibabu.

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: