Rais Magufuli Atoa Siku 14 kwa Wamiliki wa Vituo vyote vya mafuta nchini


SeeBait
Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) na atakayekiuka agizo hilo atafutiwa leseni ya biashara yake.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa KM 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.

"Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi",amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: