NEYMAR 'STAA', MESSI 'JELA', BRAZIL YAPAA, ARGENTINA PWAAA!!!


CONMEBOL
Kombe la Dunia – Russia 2018
Mechi za Makundi
Matokeo:
Jumanne Machi 28, 2017         
Bolivia 2 Argentina 0
Jumatano Machi 29, 2017         
Ecuador 2 Colombia 0
Chile 3 Venezuela 1    
Brazil 3 Paraguay 0   
Peru 2 Uruguay 1
++++++++++++++++++++++
WC-2018-SA-QUALIFIERS-1Brazil imeendelea kung'ara wakiongozwa na Staa wao mkubwa Neymar walipoifunga Paraguay 3-0 kwenye Mechi ya Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kusaka kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Wakati Brazil ikipaa kileleni na kuongoza kwa Pointi 9 mbele ya Timu ya Pili Colombia, Argentina waliporomoka hadi Nafasi ya 5 kutoka ya 3 Jana walipochapwa 2-0 na Bolivia huku wakicheza bila ya Kepteni wao Lionel Messi aliefungiwa Mechi 4 kwa kumtolea Matusi Refa Msaidizi Majuzi walipoifunga Chile 1-0.
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Siolomon Islands na Tahiti.
++++++++++++++++++++++++
Philippe Coutinho ndie aliewapa Bao la Kwanza Brazil dhidi ya Paraguay katika Dakika ya 34 na Neymar kupiga la Pili Dakika ya 63 licha ya kukosa Penati huku Marcelo akifunga la 3 Dakika ya 86.
Huko Las Paz, Wenyeji Bolivia waliichapa Argentina 2-0 iliyocheza bila Nahodha wao Messi ambae Masaa kadhaa kabla Mechi hiyo alishushiwa Kifungo cha Mechi 4.
Mechi nyingine za Argentina waliobakisha Mechi 4 za Kanda hii kufuzu Russia ambazo Messi atazikosa ni zile dhidi ya Brazil, Uruguay na Venezuela baadae Mwaka huu.
 
Bao za Bolivia zilifungwa na Juan Carlos Arce nq Marcelo Martins wakati Argentina wakimpoteza Beki wa Everton Ramiro Funes Mori alietolewa nje kwa Machela baada kuumia Goti.
Nao Colombia wamepaa hadi Nafasi ya Pili baada kuichapa Ecuador 2-0 kwa Bao za James Rodriguez na Juan Cuadrado.
Uruguay nao wamechezea kichapo cha pili mfululuzo baada Juzi kupigwa 4-1 na Brazil na Asubuhi hii kufungwa 2-1 na Peru.
Bao za Mechi hii zilufungwa Dakika za 35 na 62 kwa Peru kupitia Paolo Guerrero  na Uruguay kufunga Dakika ya 30 kwa Bao la Carlos Sanchez Arcosa lakini wakawa Mtu 10 kuanzia Dakika ya 76 baada ya Jonathan Urretaviscaya kupewa Kadi Nyekundu.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: