AMKA NA HIZI JUMANNE HII KUTOKA KATIKA VIUNGA MBALIMBALI VYA MICHEZO.


★Serengeti Boys Waendelea na mazoezi kwa Ajili ya maandaliza ya ya kuelekea nchini Gabon katika fainali za vijana chini ya miaka 17
Huku kocha mkuu wa Timu hiyo Bakarishime akiripoti kuwa kila kitu kipo sawa vijana wapo fiti na hakuna majeruhi.
★Vinara Wa ligi kuu nchini Tanzania klabu ya soka ya Simba Itawasili Leo jijini Dar es laam ikitoke jijini arusha
Kupitia afisa habari wa Simba haji s manara Amesema wachezaji wamepewa mapumziko ya siku mbili baada ya hapo wataendelea na mazoezi ili kujiandaa na michezo ya ligi kuu inakuja mbele yao.
★Taarifa Ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa klabu Ya soka ya yanga kuwa huenda wakahamishia michezo yao ya kimataifa katika uwanja wa ccm kirumba jijini mwanza huku sababu kubwa ikiwa ni Wachezaji wa yanga kushindwa kuhimili kelele za mashabiki wa simba.
★Mabingwa Wa Afrika mashariki na kati Azam fc warejea nchini
Walia na Figisu figisu walizo fanyiwa
Huko kocha mkuu wa Timu hiyo akilalamika na safu ya Ushambuliaji .
★Caf kufanya Droo Ya 32 bora michuano ya confideration barani afrika unatamani yanga Apangiwe na nani ?
SOKA KIMATAIFA
★Mchezaji Klabu bingwa Duniani Christian Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ureno wa mwaka 2016 Hongera Sana Ronaldo.
★Antonio Grizman Amesema bado yupo yupo atletico Madrid ila amesema anapendelea kucheza katika klabu kubwa kama
Madrid
Barcelona
Na Bayern Munich.
★Klabu ya Manchester united imetangaza kuwa itacheza mechi zake tano za kirafiki kujiandaa na msimu ujao wa 2017/18 huko nchini marekani
★Imeripotiwa neymar anaitamani ligi
Kuu nchini England
Ataja vilabu anavyo tamani kuchezea
Vilabu hivyo ni
Arsenal
Man u
Chelsea
Na Liverpool
★England Yazindua jezi mpya Itakayotumika
Katika kombe la dunia
Na jezi hiyo itavaliwa rasmi hapo kesho katika mchezo wa kimataifa
Wa kirafiki dhidi ya Ujerumani.

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: