ANYWA MAJI YA BETRI KWA WIVU WA MAPENZ LUDEWA

HABARI LUDEWA
ANYWA MAJI YA BETRI KWA WIVU WA MAPENZ
#LUDEWA-Njombe
MKAZI wa Kijiji cha Kimelembe wilayani Ludewa, mkoani Njombe, Maria Kayombo (31) amenusurika kifo baada ya kunywa maji ya betri kutokana na wivu wa kimapenzi.
Akizungumza na jana, mama mzazi wa mwanamke huyo Magdalena Kayombo alisema tukio hilo lilitokea juzi ambapo alipigiwa simu akiwa shambani kuwa hali ya mtoto wake ni mbaya baada ya kunywa sumu.
Alisema walimkimbiza katika zahanati ya jirani ambapo alipatiwa matibabu na kumweleza kuwa alikuwa amekunywa maji ya betri baada ya kugombana na mumewe, Peter Henjewele akimtuhumua kuwa na ‘mchepuko’.
“Sikuweza kumhoji sana kwani nilishikwa na mshangao aliponiambia amekunywa maji ya betri ili afe amuache mumewe aendelee kuwa na mchepuko,” alisema.
Akizungumzia hali hiyo baada ya kupata nafuu mwanamke huyo alisema chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo ni kitendo cha mume wake kuwa na wanawake wengine nje.
“Tulianza nae maisha katika hali ngumu, kitendo cha kuanza kuchepuka wazi wazi na wanawake wengine ni dharau nikaona bora nife kuliko kuvumilia maumivu hayo ya kimapenzi,” alisema.
Hata hivyo, mume wa mwanamke huyo, alitokomea kusikojulikana baada ya kuona mke wake amekunywa maji ya betri


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: