MICHEZO YA LIGI KUU VODACOM MWISHONI MWA WIKI



TFF-HQ-1-1Wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiendelea leo Ijumaa Oktoba 28, 2016 kwa mchezo mmoja, kwa siku ya kesho Jumamosi Oktoba 29, mwaka huu kutakuwa na michezo mitano wakati kwa siku ya Jumapili kutakuwa na michezo miwili—michezo yote ikiwa ni ya raundi ya 13, ligi ikielekea ukiongoni mwa mzunguko wa kwanza.
Leo Kagera Sugar inacheza dhidi ya Azam FC katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati kesho itakuwa ni zamu ya Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City ya Mbeya itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mwadui ya Shinyanga inatarajiwa kuialika Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu na Ndanda zitachuana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Keshokutwa Jumapili Oktoba 30, 2016 Young Africans itacheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
MECHI ZA LIGI DARAJA LA KWANZA
Mechi za Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2016/2017 zitaendelea tena kesho Oktoba 29, 2016 kwa michezo minane ya makundi A, B na C.
Katika kundi A kutakuwa na michezo miwili ambako Polisi Dar itacheza na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam wakati Friends Rangers itasafieri hadi Tanga kupambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kutakuwa pia na michezo miwili ya kundi hilo ambako Mshikamano na Ashanti zitachuana jijini Dar es Salaam kwenye kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini.
Kundi B kutakuwa na michezo mitatu kwa siku ya kesho Oktoba 29, 2016 ambako Mlale itaikaribisha Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Kurugenzi ya Mafinga itakuwa mwenyeji wa Kemondo ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uwambi huko Iringa ilhali Njombe Mji itacheza na Mbeya Warriors ya Mbeya huko Makambako.
Katika kundi hilo, KMC ya Dar es Salaam itacheza Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Kadhalika Kundi C kutakuwa na mechi tatu. Mechi hizi ni kati ya Singida United itayocheza na Polisi Mara kwenye dimba la Namfua mjini humo wakati kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Polisi itakuwa mwenyeji wa Rhino ya Tabora ilhali Panone ya Kilimanjaro itacheza na Mgambo JKT ya Tanga kwenye Uwanja wa Ushisirika mjini Moshi.
Leo Oktoba 28, kutakuwa na mchezo mmoja tu kati ya Alliance ya Mwanza itakayocheza na Mvuvumwa ya Kigoma kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
MECHI SITA LIGI YA TAIFA YA WANAWAKE
Uzinduzi wa Ligi ya Taifa ya Wanawake unatarajiwa kufanyika Novemba 1, 2016 kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika mchezo ambao Baobao itacheza na Victoria Queens ya Kagera.
Ligi hiyo ya kwanza kufanyika nchini Tanzania, lakini pia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati imetokea kuvutia wadau kadhaa wakiwamo Azam Tv ambao wamedhamini kwa kuonyesha mubashari (live), michezo hiyo 30 itakayofanyika viwanja mbalimbali.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: