Polisi Dodoma kuifua Simba SC, Jumamosi hii



Timu ya Simba SC inatarajia kushuka dimbani hapo kesho Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kumenyana na wenyeji Polisi katika mchezo wa kirafiki.
Kikosi cha Simba
Simba imeweka kambi mjini Dodoma kufuatia mapumziko mafupi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kupisha mechi za mwisho za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Wachezaji wa timu kadhaa za Ligi Kuu, hususan Azam, Simba na Yanga wamekwenda na timu ya taifa, Taifa Stars nchini Nigeria kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Nigeria huku wachezaji wengine kadhaa kutoka Azam, Simba na Yanga wa kigeni pia wakiwa wameitwa kwenye timu zao za taifa hivyo kufanya michezo yao isimame kwa muda.
Ligi inatarajia kuendelea hapo kesho kwa baadhi ya timu huku timu ambazo wachezaji wake wengi wapo timu ya Taifa zikitarajia kuendelea na ligi Septemba 07.
Katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu, Simba ilishinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC kabla ya kulazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu mwishoni mwa wiki iliyopita.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: