Timu tatu zilizopanda daraja msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania bara zimegeuka tishio kwa vilabu vikongwe katika ligi hiyo baada ya kuonehs akandanda safi na kupata matokeo ziliyoyataka.
Kikosi cha Afrcan Lyon kilichoshiriki ligi daraja la kwanza msimu uliopita
Timu hizo ni Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, Mbao FC ya Mwanza na African Lyon ya Dar es salaam.
Katika mechi za ufunguzi zilizopigwa leo, timu mbili kati ya hizo zimepata sare, na kuondoka na point 1 wakati timu moja ikipata ushindi ugenini na unyakuwa point 3.
African Lyon imeilazimisha sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam katika mchezo uliopigwa kuanzia majira ya saa 1 usiku.
Mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute, umeshuhudia African Lyon ikiing’ang’ania Azam katika muda wote wa mchezo kwa kuonesha soka la ushindani na kufanikiwa kupata bao kunako dakika ya 46, likiwa limetokana na kona ilipigwa kiufundi na Mayanja Abdul na kujaa moja kwa moja wavuni.
Azam walilazimika kuongeza mashambulizi katika dakika za mwisho na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 3 ya dakika 6 za nyongeza baada ya dakika 90 kukatika (90+3) baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Salum Abubakary nay eye kutumia uwezo binafsi kuipatia Azam bao la kusawazisha.
Katika mchezo huo, African imeonesha kandanda safi na kufanya mashambulizi mengi zaidi langoni mwa Azam katika kipindi chote cha mchezo.
Kwa upande wa Ruvu Shooting, ikichaza ugenini katika mashamba ya miwa Manungu Turiani, mkoani Morogoro, imeshuhudiwa wajeda hao wa Ruvu Shooting ikiondoka na point tatu kwa ushindi wa bao 1-0.
Mjini Shinyanga katika dimba la Kambarage, Mbao FC iliyopata nafasi ya kucheza ligi kuu baada ya vilabu kadhaa kushushwa daraja kwa upangaji matokeo, imeilazimisha suluhu ya 0-0 Stand United
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment