Manchester City wamekamilisha dili la kumsajili mshambuliaji matata Gabriel Jesus kutokea Palmeiras kwa mkataba wa miaka mitano na inaaminika kuwa ameigharimu klabu ya meneja Pep Guardioola kitita cha pauni milioni 27.
Mwenye umri wa miaka 19, ambaye alihusishwa na klabu kadhaa kubwa za Ulaya ikiwemo Manchester United, Barcelona, PSG na Real Madrid, hatajiunga na wachezaji wenzake wapya hadi mwisho wa msimu wa Brazil katika Desemba.
“Manchester City ni moja ya klabu bora duniani hivyo nafurahi kusaini,” Jesus aliambiamtandao wa klabu hiyo. “Tuna vipaji vingi vikubwa katika timu na meneja staajabu Pep Guardiola naweza kujifunza mengi kutoka kwao.
“Nataka kuonyesha mashabiki wa City ninachoweza kufanya na nadhani tutakuwa na mustakabali mkubwa pamoja.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment