Kwa waliofanya au wanaofanya kazi katika hospitali kwenye vitengo ambavyo wanaweza kuongea na kuonana na wagonjwa ambao wapo katika hali ya kukaribia kifo au walizidiwa na kushindikana kupona hivyo wanangojea kifo, wamejifunza mengi. Au kama umewahi kuwa karibu na mzee anayesubiri siku zake za mwisho kufika au mgonjwa ambaye anaumwa ugonjwa usiopona.
Katika mahospitali au kwenye watu wazee wanaosubiria siku zipite, kuna mengi sana wanaweza kutufundisha kuhusiana na maisha.
Leo tutaangalia mambo matano ambayo wengi hujutia katika dakika za mwisho kabla ya kifo.
Hii ni mojawapo kati ya kauli ambayo kuna wanakaribia kufa huzungumza. Ni kauli inayotamkwa na wengi. Katika maisha ya ujana kuelekea utu uzima wengi huishi maisha ambayo wanakuwa wamelazimishwa na marafiki, ndugu au wazazi. Wengine huishi maisha kuwafurahisha watu bila wao kupenda maisha hayo. Wengine huona raha kudanganya maisha wanayoyaishi na ikifika safari ya mwisho wa maisha hujutia sana kwa walipoteza muda wao kuishi maisha kwa jinsi watu wanavyotaka na sio kama wao wanavyotaka.
Kama unapenda kuwa daktrari kuwa daktari na sio uwe mtu wa aina nyingine wakati ndoto zako hazipo huko. Ishi katika ndoto zako na malengo yako.
Maisha yanahitaji balance. Kila kitu kina nafasi yake na umuhimu wake. Kimoja kuzidi sana huleta madhara. Ni vyema kuwa mtu wa kupangilia muda wako vyema katika kila jambo.
Wakati ni kitu cha umuhimu sana katika maisha, hivyo inatufundisha ni vyema kujitahidi kutumia muda tulio nao kuonyesha hisia zetu kwa tunaowapenda na wanaotupenda. Kama kuna matatizo omba msamaha au toa maamuzi mazuri yatakayo saidia kusuluhisha matatizo na mwisho uweze kuishi kwa amani.
Wengi huonyesha kujali mtu pale akifariki. Marafiki wa zamani watakuja kukuaga, ndugu na watu wanaokufahamu. Lakini hivi sasa hakuna anayefanya hivyo. Kila mmoja ana shughuli zake, lakini katika dakika za mwisho au baada ya maisha kuisha wengi watajitokeza kuwa wanakujua na kukupendi, hivyo ndivyo wanadamu tulivyo.
Wajali marafiki na ndugu zako. Tumia wakati huu vyema.
Wengi wanajisahau sana. Wengine wanaitafuta furaha kwa tamaa, mali, raha n.k. Mwisho ukifika wanajuta na kutamani wangeweza kuipata furaha ya daima. Furaha isiyoshikiliwa na mali, raha, thamani na anasa. Mpaka mwisho wa maisha ukifika unaanza kutambua kuwa kumbe furaha sio mali, raha, anasa, na tamaa. Bali furaha inatoka ndani mwako ukiweza kuishi kiusahihi na kuridhika na maisha na kushukuru kwa kila jambo.
Maisha ni YAKO. Hakuna mwingine anayeweza kukuchagulia maisha ya kuishi. Maamuzi unayoweka katika maisha yana adhari kwako na kwa watu wanaokuzunguka kwa kiasi fulani. Fanya maamuzi sahihi ya kimaisha, kuwa mkweli na nafsi yako. Amua kuwa na furaha hivi sasa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment