STORI: ALICHOKIFANYA HUYU MWANAMKE BAADA YA KUZIDIWA NA MUMEWE..






Wakati fulani mwaka 2005 huko nchini New Zealand mama mmoja Ng Mee Kwan raia wa Malaysia aliyekuwa na umri wa miaka 41 wakati huo alijaribu suluhu isiyo na matunda kutaka kupunguza kasi ya mchumba wake, ambaye alikuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi, kiasi kwamba, mama huyo alihisi kuwa, kuna siku atafia kitandani.

Mama huyo ambaye zamani alikuwa mhudumu wa kwenye ndege, aliamua kumtilia dawa mchumba huyo ili amvunje nguvu au kumchosha kwa lengo la kupata nafuu au kupumua. Katika malezo ya awali ya tukio hili, mama huyo alidai kwamba, mchumba wake huyo, Martin Walker, raia wa New Zealand, alikuwa akitaka kungonoka kutwa mara tano, jambo ambalo kwake lilikuwa ni mzigo mzito.

Ilidaiwa mahakamani alikofikishwa mama huyo kwa madai ya kumwekea sumu mchumbake kwenye vinywaji vyake, kwamba, alimwekea dawa kama vile, antihistamine anti-inflammatory na nyingine ili amvunje makali.

Ingawa dawa hizo siyo sumu , lakini zinapowekwa kwenye vinjwaji kama Vodka au mvinyo na hata kwenye vinjwaji baridi, kwa kiwango kikubwa, huweza kudhuru. Hata hivyo ilidaiwa kwamba, mama huyo alitumia pia sumu za kufukuzia wadudu kama mbu, kumwekea mchumba huyo kwenye chakula chake.

Alipohojiwa na Polisi awali, alisema ni kweli alikuwa anamwekea mchumbake dawa kwenye vinjwaji ili kumpooza pepo wa ngono aliyenaye. Bwana Walker ambaye uchumba wake na mama huyo umevunjika baada ya tukio hilo, amesema siyo kweli kwamba, alikuwa anataka ngono kila wakati. Hata hivyo alikiri kwamba, mahitaji yake kwenye ngono yamesababisha uchumba wao kufa, kwani mchumba wake siyo mpenzi sana wa ngono.

Hata hivyo alimtetea mwanamke huyo kwa kusema, hakuwa na lengo la kumdhuru kwa kile alichokuwa amekifanya. ‘Labda alikuwa tu anataka kupunguza kiwango changu cha hamu ya tendo ili tuweze kuendelea kuwa pamoja.’ Alisema mzungu huyo, akiwa amehuzunika.

Wakili wa Ng, amesema, mteja wake alitumia dawa hizo katika juhudi za kumpumbaza mchumbake ili asahau angalau kidogo kuhusu tendo, kwani kwake lilikuwa kama msosi. Alisema mteja wake huyo hakuwa na haja ya kumdhuru mchumbake.

Mahakama iliamua kumwachia huru mama huyo kwa madai kwamba, hakukuwa na ushahidi wa maana sana kuweza kumtia hatiani mwanamke huyo…..



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: