Rais
Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na vitendo vya rushwa
ambavyo vilinafanya jeshi hilo kukosa heshima katika jamii huku akisema
kuwa ana taarifa za jeshi hilo kuingia katika makubaliano ya kifisadi ya
mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha makamishna wa Jeshi
la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisha
kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini hadi leo hakuna
hata sare moja ya iliyonuuliwa.
Ameshangazwa
na jeshi hilo kutoa kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa kati ya
shilingi bilioni 40 hadi 60 kwa ajili ya sare za polisi ambazo hadi leo
hakuna hata moja iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi hilo likikosa
shilingi bilioni 4 tu za kukomboa magari yao zaidi ya 70 yanayoshikiliwa
na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huko bandarini.
Aidha,
Rais Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe mbele
ya haki ila angalau hata nusu ya fedha hizo ziweze kurudishwa zikalipie
magari ya polisi yaweze kutoka bandarini maramoja.
0 comments:
Post a Comment