FAIDA ZA UAMINIFU KATIKA MAHUSIANO
* Kwa kuanzia, kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuna faida nyingi kwa
mwili. Watu walio katika mahusiano bora ya mapenzi huishi maisha
marefu na kufurahia afya njema kuliko wale wasiokuwa katika mahusiano ya aina hiyo. Faida hii haina pingamizi
kwa sababu ya ukweli kwamba watu wanaokuwa katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu
fulani ambayo huwasaidia kusaidiana na kujaliana wakati wa shida. Siyo tu
kwamba watu walioko katika mahusiano ya aina hii wanaishi muda
mrefu lakini pia ni kweli kwamba wanakuwa na furaha na wanaridhika
na maisha kuliko wale wanaoshindwa kukaa katika mahusiano.
* Pili, kuwa katika mahusiano mazuri ya mapenzi kunasaidia katika mambo mbalimbali ya kimahitaji. Kusaidiana
katika mahitaji mbalimbali baina ya wapenzi ni njia nzuri ya kuwa na maendeleo. Watu wawili
wanaoshirikiana pamoja mara nyingi watakuwa na maisha mazuri zaidi ya
yule anayefanya peke yake.
Unapokuwa na mtu karibu wa kusaidiana naye katika mahitaji ni rahisi kupata mafanikio.
* Watu walio katika mahusiano mazuri wanapata msaada wa kijamii; kwa maana ya kuwa na mtu wa karibu
ambaye anajali mahitaji yako ya msingi na hisia zako. Kuwa na msaada
wa aina hii kuna faida nyingi, mojawapo muhimu ni kuweza kufanya maamuzi ya busara bila kuwa na mtindio wa mawazo na hofu ama
mashaka.
* Kuwa na mwenza katika maisha hufanya maisha kuwa ya faraja zaidi.
Kuwa na mtu ambaye mnaweza kushirikiana mambo madogo madogo
ya maisha kama kuangalia Tv, kutembea, kula pamoja ni muhimu; inaboresha mahusiano na mara nyingi watu walio katika mahusiano ya aina hii wamekuwa na maisha bora
zaidi.
* Mahusiano ni muhimu kwa sababu wapenzi wana kawaida ya kuangaliana tabia zao hasa zile ambazo ni haribifu, na wamekuwa na kawaida ya kuonyana ama kushauriana kuacha kufanya mambo mabaya na tabia mbaya. Kwa mfano
watu walio katika mahusiano ya karibu
wamekuwa na tabia ya kujaribu kuwashauri wapenzi wao kuacha
kuvuta sigara, kupunguza pombe, kuacha kutumia madawa ya kulevya
nk.
* Watu walio katika
mahusiano bora ya kimapenzi wanafanya mapenzi mara nyingi zaidi
kuliko wale walio pekee. Kufanya mapenzi mara kwa mara, kimpangilio ni muhimu kwa afya bora ya mwili na akili.
NB: ni muhimu kuzingatia kwamba kufanya huko mapenzi ambako ni bora kwa afya ya mwili siyo
kubadilisha wanaume ama wanawake, ila ni kwa mwenza wako ama mke au
mume na katika hali ya maelewano, uhuru na amani lakini pia kwa
utaratibu unaostahili ndiyo upelekea kuleta faida hiyo.
Baada ya kusema yote hayo, ni ukweli kwamba mahusiano mazuri baina ya
wapenzi huwa na faida nyingi kwa watu wenye bahati ya kupata mtu wa
kumpenda na hatimaye nao
kupendwa pia



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: