Demba Ba avunjika mguu uwanjani

 
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya ambaye sasa anaichezea klabu ya Shanghai Shenhua, Demba Ba amevunjika mguu akiwa uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya China.
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Demba Ba
Raia huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 31 alikabiliwa na mlinzi wa timu ya upinzani katika mchezo wa jana Jumapili tarehe 17 Julai.
Mshambuliaji huyo aligongwa mita chache tu kabla ya kisanduku cha hatua 18 na alipoanguka mguu wake ulipinduka kwa hali isiyo ya kawaida na kuvunjika papo hapo.
Aidha kocha wa klabu yake Gregorio Manzano amesema kuwa tukio hilo linaweza kumlazimisha nyota huyo kustaafu kucheza soka.
Ba aliwahi kuichezea West Ham, Newcastle na Chelsea zote katika ligi kuu ya Uingereza kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Uchina akitokea Uturuki katika klabu cha Besiktas.
Msimu huu Ba anaongoza orodha ya wafungaji mabao akiwa na jumla ya mabao 14 katika mechi 18 alizoshiriki.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: