LUDEWA WAGOMEA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMI

Ludewa

Wananchii wa kijiji cha Ludewa mjni kata ya Ludewa wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wamekataa kupokea Taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji hicho kwa kuwa taarifa hiyo haija kidhi kiwango cha kuitwa taarifa ya kuwapa wananchi ili wairidhie.

Wakiwa mkutanoni hapo baadhi ya wananchi walio shiriki mkutano uliofanyika eneo la ofisi ya kaya ya Ludewa wananchi hao wamelaani vikali tendo la mhasibu wa kijiji hicho0 kuwapa taarifa ambayo haina mchanganuo wowote wa matumizi ya fedha za kijiji hicho kama hapa taarifa inavyoonesha👉.

Aidha wananchi hao wameainisha baadhi ya sababu zilizo sababisha wasipokee taarifa hiyo kuwa ni pamoja na Taarifa hiyo kutokuwa na Jina la kijiji,Taarifa haijaonesha madeni ya kijiji,vilevile wananchi hao wameshangazwa na tendo la baadhi ya vyanzo vya mapato kuonesha fedha kidogo wakat siyo hivyo ikiwa ni pamoja na chanzo cha mapato cha kuni na mikorogo ya pombe.
[4/20, 10:31] IG: Katika hatua nyingine wananchi hao wameshangazwa kuambiwa kijiji hicho hakina hati ya kijiji huku wakimtaka mwenyekiti wa kijiji hicho kufuatilia hati ya kijiji hicho haraka iwezekanavyo ili kuonekana kijiji halali.

Wananchi wameongeza kuwa suala la mapato na matumizi kuto kamilika ni suala la kawaida kwa kijiji cha Ludewa mjini huku wakisema tatizo huwa linajitokeza kila mkutano na wananchi kutoridhia taarifa hiyo na kuikataa kabisa.

Mara baada ya Agenda ya mapato na matumizi kuto kamilika kwa mikutano zaidi ya miwili wananchi hao wamesema viongozi wa kijiji wanafanya kazi kwa mazoea na wanafanya kwa kuwadanganya wananchi hivyo basi wamewaagiza viongozi wa kijiji hicho ambacho ni hewa hakina hati kumwomba semina ya wahasibu mkurugenzi wa H/ ya wilaya ya Ludewa




 yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: