Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya ambayo inachezewa na golikipa wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga Juma Kaseja, mchana wa March 28 imeamua kuweka taarifa sawa kuhusiana na tetesi au uvumi uliokuwa unasambazwa mtandaoni kuhusu Kaseja.
Mbeya City imetumia ukurasa wake wa instagram, baada ya kuzipata taarifa zisizo za kweli kuhusu uvumi kuwa golikipa wao Juma Kaseja amefariki Dunia, ukweli ni kuwa huo ni uzushi uliotungwa na watu, Juma Kaseja ni mzima na leo amefanya mazoezi na timu.
Hii ndio post ya Mbeya City iliyotoa ufafanuzi kuhusu tetesi hizo.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment