.
Epuka kuweka kilevi au pambe nyumbani au sehemu ya kazi ili kuepuka majaribu.
Usipende kuruka mlo, kula chakula mara tatu (3) mpaka mara nne (4) kwa siku ili kuupatia mwili virutubisho vyote muhimu.
Ondoa dhamira potofu kwamba huwezi kuishi pasipo kunywa pombe. Kumbuka mwili wako umeumbwa kikamilifu kukabili hali zote za maisha, hivyo usihisi kuwa pombe ndio kichochea chako kila unapotaka kufanya jambo fulani.
Zingatia mlo kamili, na jifunze kula matunda kwa mwingi. Hasa kama ulikuwa huli.
Anza kufanya mazoezi na upange ratiba yako ule muda ambao ulikuwa ukitumia kunywa pombe.
Kumbuka mambo mabaya yaliyokutokea kutokana na pombe katika maisha yako. Hii itakusaidia kutothubutu tena kunywa pombe.
Ongeza unywaji wa maji, jiwekee mazoea ya kunywa maji angalao glasi tano (5) kwa siku.
Kuwa na tabia ya kujizawadia/kujipongeza kutokana na uamuzi wako mzuri wa kutokunywa pombe.
Ni muhimu kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki wa karibu kuhusu uamuzi wako wa kuacha pombe/kileo na pia usijione mjinga kwa wale watakao kucheka.
PANAPO MAJALIWA.KAPULYA WENU
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment