AFCON 2017- KUNDI LA TANZANIA: EGYPT YAITUPA NJE NIGERIA, TANZANIA BADO MATUMAINI....!!!




AFCON2017-SIT-LOGOJana huko Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria, Wenyeji Egypt waliifunga Nigeria 1-0 katika Mechi ya Kundi G la Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, na kujiweka pazuri mno kutinga Fainali huko Gabon 
Matokeo hayo yamewatupa nje Nigeria kutoka Mashindano haya wakiwa wamebakisha Mechi 1 ya Kundi G ambalo  limebaki Timu 3 baada ya Juzi Chad kujiondoa na matokeo ya Mechi zao kufutwa kwenye hesabu.
Bao la ushindi la Egypt hapo Jana lilifungwa Dakika ya 62 na Ramadhan Sobhy.
Sasa Egypt wanahitaji Sare tu katika Mechi yao ya mwisho Jijini Dar es Salaam dhidi ya Tanzania ambayo bado inayo matumaini ya kufuzu ikuwa itashinda vizuri Mechi zake 2 zilizobaki na kutwaa ushindi wa Kundi G au kupita kwa Tiketi ya Mshindi wa Pili bora.
Kwa Nigeria ambao hawawezi tena kutwaa ushindi wa Kundi G kilichobaki ni kuomba miujiza ya kufuzu kwa moja ta Tiketi 2 za Mshindi Bora wa Pili.
Kwenye Kundi F, Morocco iliichapa 2-0 huko Marrakesh na kuwa Timu ya kwanza kufuzu Fainali za AFCON 2017 huko Fabon huku ikiwa na Mechi 2 mkononi.
Bao za Morroco zilifungwa na Youssef El Arabi.
KUNDI G - MSIMAMO:
Egypt Mechi 3 Pointi 7
Nigeria Mechi 3 Pointi 2
Tanzania Mechi 2 Pointi 1
**Chad ilijitoa ( Matokeo ya Mechi zake yamefutwa)
++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2017
MAKUNDI:
KUNDI A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
KUNDI B: Madagascar, DRC, Angola, CAR
KUNDI C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
KUNDI D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
KUNDI E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
KUNDI F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
KUNDI G: Nigeria, Egypt, Tanzania, Chad
KUNDI H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
KUNDI I: Cote d’Ivoire, Sudan, Sierra Leone, Gabon
KUNDI J: Algeria, Ethiopia, Lesotho, Seychelles
KUNDI K: Senegal, Niger, Nambia, Burundi
KUNDI L: Guinea, Malawi, Zimbabwe, Swaziland
KUNDI M: Cameroon, South Africa, Gambia, Mauritania
MFUMO:
-Makundi yapo 13 ambapo 12 yana Timu 4 na moja lina Timu 3 lakini Wenyeji Gabon, ambao wanafuzu moja kwa koja kucheza Fainali, wamechomekwa Kundi hilo [KUNDI I] ambapo Mechi zao ni za Kirafiki tu.
-Mshindi wa kila Kundi [Washindi 13] na Timu 2 zitakazomaliza Nafasi za Pili Bora zitatinga Fainali kuungana na Wenyeji Gabon na kufanya Jumla ya Timu 16.
++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2017
Matokeo
Jumanne Machi 29
Angola 0 Congo DR 2 
Egypt 1 Nigeria 0
South Africa 0 Cameroon 0
Malawi 1 Ghana 2
Lesotho 2 Seychelles 1
Rwanda 5 Mauritius 0
Ethiopia 3 Algeria 3
Togo 0 Tunisia 0
Namibia 1 Burundi 3
Uganda 0 Burkina Faso 0
Liberia 5 Djibouti 0
Angola 0 Congo DR 2
Gambia 0 Mauritania 0
Sudan 1 Ivory Coast 1
South Africa 0 Cameroun 0
Morocco 2 Cape Verde 0
MSIMAMO WA MAKUNDI:
NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: