Nchi ya Uingereza ina sheria kali hasa ya masuala ya ndoa za utotoni hii ni pamoja na kuwabana watu wazima wanaojihusisha na masuala ya ngono kwa watoto walio chini ya miaka 18. Tayari mchezaji wa zamani wa Manchester City na timu ya Taifa ya Uingereza, Adam Johnson amehukumiwa miaka sita kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15.
Hukumu dhidi ya mchezaji huyo imetolewa mapema jana Machi 24.2016 wakati alipopandishwa kizimbani juu ya kesi yake hiyo. Adam Johnson hadi anahukumiwa kifungo hicho alikuwa anaitumikia klabu ya Sunderland ya Uingereza, ambayo toka mwaka 2012 alijiunga nayo hadi 2016, ameichezea jumla ya mechi 122 na kuifungia magoli 19.
Katika kesi hiyo, mchumba wake wa zamani aliweza kumsindikiza Mahakamani hapo kama njia ya kumsaidia kutoa ushahidi, ambapo hata hivyo mwisho wa siku hukumu ikatoka na kwenda jela miaka hiyo sita.
Awali imeelezwa kuwa, Star huyo wa soka alikuwa akijihusisha na mapenzi na binti huyo mdogo ambaye ni Mwanafunzi, ambapo meseji ya mwisho iliyosababisha utata hadi kupelekea kutiwa hatiani, Adam Johnson alimtumia binti huyo kwa kumbusu (Kissing) na mambo ya kimapenzi kupitia mtandao wa Kijamii wa WhatsApp na baada ya dakika 15, aliweza kumtumia mpenzi wake huyo kumpongeza kwa kupata mtoto, Hata hivyo Adam Johnson na wanasheria wake wanaendelea kumkosoa mchumba huyo wa zamani kuwa ndiye aliyetoa siri.
Tazama hapa kuona tukio hilo:
Mchezaji Adam Jahnson akiwasili Mahakamani..
Mchumba wa zamani wa Adam Jahnson, Bi.Stacey Flounders akiwasili Mahakamani
Adam Jahnson akisindikizwa kwenda jela mara baada ya hukumu kutolewa..
Adam Johnson na timu yake ya Sunderland ambayo alikuwa anaichezea kabla ya kupata hukumu hiyo iliyotolewa jana Machi 24.2016.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment