ROBO FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND
Man Utd Vs West Ham
Reading Vs Crystal Palace
Everton Vs Chelsea
Arsenal/Hull City Vs Watford
KOCHA Louis Van Gaal 'amepumua' kidogo baada ya Manchester United kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la FA England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Shrewsbury Town Uwanja wa New Meadow. Shukrani kwao, wavungaji wa mabao hayo, Chris Smalling dakika ya 37, Juan Mata dakika ya 47 na Jesse Lingard dakika ya 61.
Kwa ushindi huo, Mashetani Wekundu watamenyana na West Ham United na West Ham United Uwanja wa Old Trafford mwezi ujao.
Robo fainali nyingine, Chelsea itaifuata Everton katika Robo Uwanja wa Goodison Park, kufuatia kuitoa Manchester City kwa kuifunga mabao 5-1 usiku wa leo Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Crystal Palace ya mshambuliaji wa Togo, Emmanuel Adebayor itasafiri kuifuata Reading baada ya kuitoa Tottenham Hotspur leo kwa kuifunga 1-0 Uwanja wa White Hart Lane.
Watford itasafiri kuifuata Arsenal au Hull City, wakati West Ham United itasafiri kuifuata Shrewsbury Town au Manchester United.
Arsenal watarudiana na Hull City kusaka timu ya kwenda Robo Fainali, baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates jana, wakati Shrewsbury Town wataikaribisha Manchester United kesho Uwanja wa New Meadow kuanzia Saa 4:45 usiku.
Man Utd Vs West Ham
Reading Vs Crystal Palace
Everton Vs Chelsea
Arsenal/Hull City Vs Watford
Wachezaji wa Manchester United wakimpongeza mwenzao, Juan Mata (katikati) baada ya kuifungia timu yake kwa shuti la mpira wa adabu usiku wa Jumatatu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kwa ushindi huo, Mashetani Wekundu watamenyana na West Ham United na West Ham United Uwanja wa Old Trafford mwezi ujao.
Robo fainali nyingine, Chelsea itaifuata Everton katika Robo Uwanja wa Goodison Park, kufuatia kuitoa Manchester City kwa kuifunga mabao 5-1 usiku wa leo Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Crystal Palace ya mshambuliaji wa Togo, Emmanuel Adebayor itasafiri kuifuata Reading baada ya kuitoa Tottenham Hotspur leo kwa kuifunga 1-0 Uwanja wa White Hart Lane.
Watford itasafiri kuifuata Arsenal au Hull City, wakati West Ham United itasafiri kuifuata Shrewsbury Town au Manchester United.
Arsenal watarudiana na Hull City kusaka timu ya kwenda Robo Fainali, baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates jana, wakati Shrewsbury Town wataikaribisha Manchester United kesho Uwanja wa New Meadow kuanzia Saa 4:45 usiku.
Mechi za Robo Fainali za Kombe la FA zitachezwa wikiendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment