Mreno, 53, ambaye alitupiwa virago na Blues mwezi Desemba, anaendelea kuwa na matumaini ya kumrithi Louis van Gaal Old Trafford.
Mourinho alifukuzwa kazi Chelsea mwezi Desemba 2015
Hakuna makubaliano yaliyofiki, na klabu haijatamka lolote, lakini makubaliano yameanza.
Mholanzi Van Gaal, 64, anatarajiwa kuondoka United mwishoni mwa msimu – mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.
Louis van Gaal wa Manchester United anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.
Hiyo itamuwekea njia wazi Mourinho, ambaye anajulikana kuwa atafurahia endapo ataichukua Old Trafford
0 comments:
Post a Comment