Vinara wa EPL Leicester City wametoa tena dozi ya kutosha walipokutana na Manchester City na kuibuka na ushindi wa maana wa bao 3-1kwenye dimba la Etihad na kuendelea kutesa kileleni mwa ligi kwa pointi sita mbele ya wapinzani wao wa karibu Man City.
Manchester City walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini safu yao ya ushindi ilijikuta ikiadhibiwa na vilivyo kwa makosa waliyofanya mbele ya Leicester.
Robert Huth amepiga bao mbili kwenye game hiyo huku Riyad Mahrez akipiga bao moja wakati huo akiwa amepika moja ya bao ambalo lilifungwa na Huth
Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao pekee la kufutia machozi dakika za lala salama.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment