Leo
kwenye safu hii nimekuja na mada ambayo itawagusa wasichana wengi ambao
uhamia kwa wanaume wanaowapenda na kuishi nao bila hata ya kujali kuwa
dini hairuhusu.
Utakuta
msichana anaanza kwenda kutembea kwa mpenzi wake wa kiume kwa
kujifichaficha sana, anaanza kwa kutafuta visababu vidogovidogo mara
anaacha rangi ya mdomo, siku inayofuata anaenda na pea mbili za viatu
anaacha moja akijifanya amesahau.
Siku
inayofuata tena ataamua kuongeza shuka kwani ataona shuka nyumbani kwa
bwana hazitoshi, taratibu mwisho atahamishia kabati zima la nguo.
Hiyo
haitoshi ataanza kwa kumnunulia vikombe mpenzi wake naye ataweka cha
kwake mwisho wa siku kabati nalo litajaa vyombo kama vile tayari kaolewa
anahudumia kwa mume.
Hii
ni mbaya sana akina dada kwani inashangaza kuona mmeamua kujimilikisha
wanaume kabla hamjaolewa, hivi hamuoni kila kukicha dharau ndiyo
zinazidi mpaka ndoa siku hizi hazipewi kipaumbele kama zamani, unajua ni
kwa nini? Kwa sababu wanaume wakitaka wanawake wanawapata kirahisi.
Nani wa kulaumiwa
kwa haya?
Kwa
haya anayetakiwa kulaumiwa ni wazazi wa binti, baadhi ya wazazi
wamekuwa wakikubaliana na hali ya watoto wao kuhamia kwa wanaume kwani
akirudi nyumbani anampokea kama kawaida bila kumuuliza alikuwa wapi.
Wengine
wanapokea hata hela wanazoletewa na binti kutoka kwa mwanaume husika na
mtoto akitaka kwenda kulala anamuaga mama na kumuacha amekaa sebuleni
bila kujiuliza ni kwa nini mwanangu ameamua maisha haya au hata kuwa
mkali basi maana mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Kinachouma sasa
Kinachouma
kwa mabinti zetu hata ukiamua kuhamia kwa mume unakuwa huna cha kushika
wala huna haki yoyote akiamua kukufukuza muda wowote anakufukuza kwani
hana ndoa na wewe.
Je, utamshtaki wapi?
Kumbuka
kuwa huna pa kumshtaki kwani hata ikitokea mmegombana ugomvi wenu pa
kukimbilia huna kwa sababu uhusiano wenu siyo rasmi.
Ikitokea maafa mko
wote ndani?
Hivi
ujiulize ikitokea maafa uko ndani na mpenzi wako halafu amefariki dunia
na wazazi wake hawakujui utafanya nini? Huoni kama utakosa pa kuanzia
na huenda kesi ikawa ya kwako.
Kwa leo nimeona niwakumbushe hili kwani naona ni kama fasheni wasichana kuhamia kwa wapenzi wao.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment