WAKUBWA MPOO!!! HIIN NI CHEMBA YENU TWENDE MZIGO;;DHANA YA KURIDHISHANA!!!! CHONDE CHONDE HILI SOMO HALIWAHUSU WENYE CHINI YA MIAKA18.





Kiukweli ni mada ya ndani sana, lakini nitatumia zaidi tafsida kufikisha ujumbe kwa walengwa pekee.

Yes...kuna hiki kilio cha kutofurahishana kimahaba
kati ya wapenzi wanapokuwa faragha.
Sioni haya kusema kwamba, wengi wanaokabiliana
na tatizo hili ni wanawake! Yaani hawa wapo wengi
sana ambao hata ile raha ya mapenzi yenyewe hawaijui! Wanabaki kusikia kwa mashoga zao tu,
wanapokwenda salon.


Hakuna shaka kwamba, msingi mkuu wa ndoa,
baada ya upendo ni tendo lenyewe la ndoa. Hiki
ndicho hasa kinachowaunganisha, maana hata hao
watoto wanapatikana kwa njia hii.

 “Nina miaka saba ya ndoa, tunao watoto wawili na
mume wangu, lakini kiukweli kabisa, sijawahi
kufurahia mapenzi hata siku moja, nafikia mahali
nawaza kutafuta mwanaume mwingine nje,”
anasema mama Helena, mkazi wa Soweto, Mbeya
kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno. 


Mama Shamanona wa Dodoma anasema: “Mr. akija
anakuwa na miharaka yake, tunakutana
harakaharaka, akimaliza haja zake anakoroma,
ananiacha nateseka, nimeshavumilia nimechoka,
nimeona ni bora nitoe dukuduku langu kwako
mshauri unaweza kuwa na mawazo ya kunisadia.” Wapo wengi, lakini hao ni baadhi yao tu.


 Je,
unadhani ni sahihi wanawake hao watafute
wanaume wengine nje ya ndoa zao kwa ajili ya
kusaka penzi bora? Penzi bora ni lipi hasa? Ni
usaliti? Majibu ya maswali yote hayo hapo ni
kwamba si sahihi! Moto hauzimwi kwa moto, bali maji.


Tatizo huwa
halikimbiwi wala kuhairishwa, isipokuwa hutafutiwa
njia za utatuzi. Hiyo ndiyo njia sahihi ya kukabiliana
na tatizo. Hebu kwanza tuone maana ya
kuridhishana, halafu tuendelee na vipengele vingine.
DHANA YA KURIDHISHANA! Katika mapenzi ni vizuri wote mkatoka mkiwa
mmekata kiu zenu ipasavyo.


 Hakuna mapenzi ya
upande mmoja! Si kweli kwamba wanaume pekee
ndiyo wanaotakiwa kumaliza haja zao na kuwaacha
wanawake wakiwa bado wanawahitaji!
Baadhi ya mila za makabila fulani, huzingatia hili, kwamba mwanamke hana uwezo wa kumwambia
mumewe; “Sijaridhika.”


Akifanya hivyo, anaweza kupigwa lakini pia
ataonekana kama mwanamke asiye na staha. Hiyo
si sahihi, kama ilikuwa zamani, katika kizazi kipya
haitakiwi kupewa nafasi kabisa.


 TATIZO LIPO WAPI HASA?
Vipo vitu vingi sana vinavyochangia tatizo la
kutoridhishana faragha. Hapa nitachambua
machache, ambayo angalau yatakupa mwanga na
kukufanya ujue upo kwenye kundi gani, halafu
baada ya hapo, nitakupa dawa ya moja kwa moja ya tatizo hili.


(i) Utayari kisaikolojia
Pamoja na mambo yanayoweza kusababisha
kushindwa kuridhika faragha, utayari kwa
kisaikolojia unatajwa kushika nafasi ya juu zaidi.
Yapo matatizo mengi, lakini kutolewa usichana kwa njia ya ubakaji ni kati ya sababu hizo. Mwanamke
anapobakwa huwa haridhiki na kinachotokea pale ni
maumivu, hivyo kuanza kuchukia kabisa tendo hilo.
Kama mwanamke huyo hatapata ushauri mzuri wa
wataalamu mapema, anaweza kupatwa na tatizo
hili.


 (ii) Mawazo
Kushinda kutwa nzima mara nyingi kwa mtindo wa
kujiinamia, kunatajwa pia kama sababu ya
kutofurahia mapenzi na si kufurahia tu bali hata
kuondoa kabisa hamu ya tendo hilo.
Inashauriwa, kujitahidi kadri ya uwezo wako wa mwisho kuhakikisha tabasamu linakuwa sehemu ya
maisha yako. Kuwa na furaha ni jambo jema, kwani
zaidi ya kuchangamsha ubongo, mwili unakuwa
katika msisimko wa kufurahia mapenzi.


(iii) Ukali
Kama upo kwenye uhusiano na mwenzi ambaye muda wote anakuwa mkali, hilo ni tatizo lingine
litakaloweza kukupunguzia ari ya kufanya na
kufurahia tendo la ndoa.
Mwanaume ambaye muda wote ni mkali, mgomvi,
mwenye masimango, anachangia kwa kiasi kikubwa
mwanamke kumuogopa na kukosa utayari wa tendo lenyewe, mwisho anakuwa haridhiki na tendo
lenyewe.


(iv) Mazingira
Ndiyo...mazingira yanaweza kabisa kusababisha
mwanamke asifurahie mapenzi. Mathalani anaishi
ukweni, ndugu zake au kwenye nyumba ndogo ambayo inaweza kuruhusu watu wa chumba
kinachofuata kusikia kila kitu katika chumba chao.
Kikubwa hapa ni woga au aibu, kwani huwaza zaidi
jinsi atakavyofedheheka atakapokutana na watu hao
mitaani. Hili linatosha kabisa kupoteza hamu ya
tendo au kutoridhika akiwa na mwezi wake faragha. 


(v) Maandalizi
Huwezi kumla kuku akiwa mzima, lazima achinjwe,
atayarishwe na kubandikwa jikoni, huo ndiyo
utaratibu uliopo hata kwenye suala la mapenzi.
Wanaokurupuka ndiyo husababisha wenzi wao
kutofurahia mapenzi. Sina shaka umepata kitu kipya kichwani mwako.
Umegundua upo katika kundi gani, hapo sasa ni
hatua nzuri zaidi ya kuelekea kwenye kujua namna
ya kufanya ili kukabiliana na tatizo hili. Natamani
sana kuwapa dawa hiyo leo, lakini kutokana na
nafasi yangu finyu, nalazimika kuishia hapa



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: