TASWIRA YA SAMATTA ALIVYOMUONYESHA KIKWETE TUZO YAKE, NAYE AKAMKABIDHI JEZI YA TP MAZEMBE



Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta leo amemkabidhi jezi yake Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Samatta alikwenda kumtembelea Kikwete katika makao makuu ya CCM ambayo yeye ni mwenyekiti wake na kumshukuru kutokana na mchango wake wakati akiwa Rais wa Tanzania.


Baada ya kumuonyesha tuzo yake ya Mwanasoka Bora Afrika ndani ya Afrika, Samatta alimkabidhi Kikwete jezi namba 9 anayoivaa Mazembe. Alifanya hivyo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.




Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na straika Mbwana Samatta ambaye anaendelea kupokea pongezi za Watanzania kwa ushujaa wa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Wanaocheza Ndani ya Afrika, wiki iliyopita.

Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amempongeza kwa mafanikio hayo lakini akatoboa siri kuwa yote ni  matokeo ya wosia aliyompa walipokutana mjini Kinshasa, DR Congo ambapo alimtaka awaze mafanikio ya juu zaidi hasa Ulaya badala ya kujiona kama amefika akiwa na kikosi cha TP Mazembe.

Katika mkutano na waadishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Rais JK alisema ana kila sababu ya kumpongeza straika huyo ambaye anaelekea Genk ya Ubelgiji kama mambo yote yataenda sawa kwani ndiye mkombozi wa taifa ambalo limekuwa na ukame kwenye michezo huku akiiomba wizara ya husika ya michezo kuhakikisha wanamsaidia katika kila hatua.

“Tanzania tumekosa furaha muda mrefu kwenye michezo, tumekosa makombe miaka mingi, lakini Samatta leo hii ametuinua kwa kuleta tuzo hii. Lazima tumpongeze.

“Nilikutana naye Kinshasa nilimisihi sana alenge juu zaidi na sio Mazembe na shabaha kubwa iwe ni Ulaya ili nasi siku moja tumuombe kwenye runinga akicheka na nyavu. 

"Alitekeleza nilichomwambia na kweli timu nyingi leo hii zinamtaka huko Ulaya. Nimeomba wizara ya michezo waone jinsi ya kumsaidia katika kila hatua atakayopiga,” alisema Rais JK.

Kwa upande wa Samatta amempongeza JK na serikali ya awamu ya nne kwa kuwa naye bega kwa bega kwa kila hatua aliyoipiga.

Aidha, Samatta alimkabidhi Rais JK zawadi ya jezi ya TP Mazembe No 9 aliyokuwa akivaa klabuni hapo ambayo anaiacha baada ya kupata dili Ubelgiji anakoelekea sasa.





Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: