Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bi.Hawa Ng'humbi amewaagiza wakuu wa idara katika halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha watu wote watakaowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa mahakamani mara moja kwakuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka siku baada ya siku wilayani humo hali inayorudisha nyuma jitihada za kukuza kiwango cha elimu nchini.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Idukilo wilayani Kishapu Shinyanga baadhi ya wananchi wamemtaka mkuu wa wilaya ya Kishapu Bi.Hawa Ng'humbi kufuatilia kwa karibu zaidi swala la mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekua kero inayodumaza elimu katika kata hiyo huku baadhi ya wazazi wakiendelea kuwaozesha watoto wakike wakati wakiwa wadogo kwa lengo la kujipatia mali.
Awali katika mkutano huo mkurugenzi wa shirika la Agape linaloshughulika na haki za watoto wa kike Bw.John Myola amedai kuwa rushwa iliyokithiri kwa watumishi wa serikali imekuwa chanzo kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni hali ambayo isipodhibitiwa mapema taifa litaendelea kupoteza nguvu kazi kwa ongezeko la vifo vya wanawake na watoto wachanga wakati wa kujifungua.
Akitoa maagizo kwa wakuu wa idara, watendaji wa kata na vijiji pamoja na wazazi Bi Hawa Ng'humbi amesema yeyote atakayebainika kumpa mimba mtoto wa kike afikishwe mahakamani maramoja ili hatua za kisheria zichukuliwe huku akilipongeza shirika la Agape kwa jitihada kubwa za kumkomboa mtoto wakike ambapo alipokea vyerehani vitano kutoka shirika hilo na kuwakabidhi baadhi ya wasichana waliokuwa wamekatizwa masomo yao baada ya kupata mimba na kuacha masomo yao.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment