Serikali
ya rais John Magufuli imeendeleza kasi iliyoanza nayo na hivi sasa
imeonesha kuanza kuufanyia kazi kwa vitendo ujenzi wa barabara
zinazopita juu (flyovers) jijini Dar es Salaam ili kuondoa adha ya
foleni za magari.
Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco), limeanza kufanya kazi ya kuhamisha nyaya
za umeme zilizokuwa zikipita karibu na barabara katika maeneo ya uwanja
wa ndege, karibu na kituo kidogo cha kuzalisha umeme cha Kipawa chenye
KV 33.
Meneja
wa Tanesco Mkoa wa kitanesco wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali
amekieleza kituo cha runinga cha Star TV kuhusu utekelezaji wa zoezi
hilo.
“Tumeanza
wiki mbili zilizopita, na leo tumeshahamisha kwa asilimia 90. Baada ya
wiki mbili tutawatangazia wananchi tutazima umeme tumalizie hii portion
iliyobaki,” alisema na kuongeza kuwa baada ya hapo watahamia katika
maeneo mengine.
Ujenzi
wa flyover unatarajiwa kufanyika katika eneo la makutano ya barabara za
Nyerere na Mandela na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi
35.
Akiwa
bado ni waziri wa ujenzi, Mwezi Oktoba mwaka jana, Dk. Magufuli
alisaini mkataba wa ujenzi wa flyovers na kampuni ya kandarasi ya
Sumitomo Mitsui Construction na aliahidi kuhakikisha ujenzi huo
unatekelezwa kivitendo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment