|
NIMETUMIWA NIMESHARE LADIES HII NI ZAWADI Ni msichana mmoja ambaye alikutana na mwanaume kwenye Mtandao wa kijamii unaoitwa Badoo, katika kipindi chote hicho wanachati yule Jamaa alikuwa Nigeria na yule msichana alikuwa Mombasa Kenya, Jamaa alionyesha nia nzuri sana kwa yule msichana kwani walizungumza mengi kiasi cha kufikia malengo ya kuishi wote hapo baadaye, yule mwanaume alionyesha kujali sana, na kumtumia fedha nyingi sana yule dada kupitia Money gram na western union, "demu akawa anakula Bata mbaya, starehe za Hapa na pale, kila weekend viwanja vyote vya Bata vinamjua" alikuwa na pesa nyingi sana zaidi ya sana na kujiita lile jina la-"the Boss lady" kama unavyojua siku hizi dada zetu, akiweza kuingiza 10,000 kwa siku tu, anajiita 'Boss Lady' Baada ya miezi kadhaa ndio yule M Nigeria akamtumia Ticket ya Ndege ili yule Dada aende Lagos Nigeria, Yule dada nae ikabidi amtafute best friend wake ili waende wote! Yule Jamaa kwa kuwa alikuwa na uwezo akatuma ticket mbili. Safari ikaanza kutokea Kenya kulekea Nigeria, walipofika Nigeria, yule Jamaa alikuwa akiwasubiri Air port kuwapokea. Yule demu na mwezake walipoona Jamaa kapaki Gari aina ya Escalade Jeep walitahamaki, na kuanza kukonyezana "mmh, shoga Hapa kuna pesa hapa" Walipofika nyumbani kwa yule Jamaa majira ya saa moja hivi usiku! Ndio ikabidi yule Dada akapumzike na yule M Nigeria faragha, Yaani wakawa private room wamepumzika, na yule mwingine akalala chumba kinachofuata! Usiku kama Mida ya saa saba akasikia makelele yanatokea Chumbani kule walipolala wappendanao hao, hakuchukulia maanani kwani alijua labda wanafanya matusi sasa yule dada Labda ndio anakolezwa! Lakini cha ajabu alisikia kelele nyingi halafu za kuomba msaada na kutaja jina la rafiki yake! "Nisaidie Naomi, nakufa uwiiiiiiiiiiii, mamaaaaweeee....!" kelele zilisikika. Naomi ikabidi akurupuke, na kutafuta mbinu za kuvunja mlango. Alifanikiwa kuvunja mlango ingawa alitumia takribani kama dakika 50 hv Ghafla alimuona nyoka mkubwa ndio anamaliza kummeza rafiki yake, Naomi aliishiwa nguvu. Akaanza kukemea" lile Joka likawa linamtazama Naomi kwa ghadhabu sana, na kujilamba lamba, Naomi alianguka chini nakuzimia hapo
|
Ludewa yetu na maendeleo yetu
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment