SALIM (KUSHOTO) AKIONGOZA MAZOEZI YA SIMBA |
Katika kile kilichoonekana kuwa ni hasira ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi jana, Kocha wa Makipa wa Simba, Abdul Salim, alijikuta kwenye wakati mgumu na huenda alilala lupango baada ya kukamatwa na polisi kwenye Uwanja wa Amaan.
Kocha huyo raia wa Kenya alikamatwa na polisi kufuatia kumshushia kipigo shabiki mmoja ‘waliyezinguana’ naye baada ya Simba kufungwa na Mtibwa bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali.
Baada ya kocha huyo kumpiga shabiki huyo, polisi walimkamata na kumweka kwenye ‘difenda’ kisha wakaondoka naye.
Baadaye viongozi wa Simba walikuwa wakihaha kutaka kujua alipokuwa amepelekwa kwa lengo la kumuwekea dhamana.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment